METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 19, 2021

MWALIKO WA KUTOA MAONI KWENYE MAREKEBISHO YA KANUNI ZA UTANGAZAJI NA MAUDHUI MTANDAONI

Dodoma

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa,  anawakaribisha wadau wa Sekta ya Habari nchini hasa wanaojihusisha na Huduma  za Utangazaji na masuala ya utoaji maudhui kwa Umma kupitia mitandao, redio na televisheni kutoa maoni katika Rasimu ya Marekebisho ya Kanuni za Maudhui  Mtandaoni za Mwaka 2020 pamoja na Kanuni za Maudhui ya Utangazaji katika  Redio na Televisheni za Mwaka 2018. 

Marekebisho haya yamefanywa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 165 cha Sheria ya Mawasiliano ya  Kielektroniki na Posta ya mwaka 2010. Maboresho hayo yatazifanya Kanuni hizo ziendane na maendeleo ya teknolojia pamoja na kuongeza wigo wa upatikanaji wa  habari kwa wananchi. 

Rasimu za marekebisho ya Kanuni hizo zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara  (www.habari.go.tz) pamoja na tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA (www.tcra.go.tz). 

Maoni yawasilishwe kwa anuani za barua pepe zifuatazo: hglsu@habari.go.tz na  amina.nguli@habari.go.tz.  

Pia, Wizara inawakaribisha wadau wa huduma za utangazaji nchini kufika katika  mkutano wa wadau Agosti, 26, 2021, katika Ukumbi wa PSSSF (Zamani – LAPF)  Jijini Dodoma, kuanzia Saa 2.00 Asubuhi ili kuhitimisha zoezi la utoaji maoni. Wote  mnakaribishwa. 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com