Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka (katikati) na viongozi wengine wakionesha nakala ya Jarida
la Msaada wa Kisheria lililozinduliwa katika Kilele cha Maadhimisho ya
Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika
Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21,
2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Msajili wa Taasisi za watoa
huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi.
Felistas Mushi, katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa
Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa Katika Uwanja wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa mkoa mkoa huo(hawapo pichani),
katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25,
2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa
Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo
pichani), katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria
Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka(kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jarida la
msaada wa kisheria katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa
Kisheria Oktoba 25, 2019 yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya viongozi wa Mkoa huo na wataalam wa Sheria kutoka Wizara ya
Katiba na Sheria na taasisi za watoa huduma za kisheria, katika Kilele
cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Oktoba 25, 2019
yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi
mkoani Simiyu kuanzia Oktioba 21, 2019.
………………………
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Msajili wa Taasisi za watoa
huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi.
Felistas Mushi amesema takribani wananchi 1018 wamepata huduma ya
msaada wa kisheria katika maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria
tangu Oktoba 21, 2019 mpaka Oktoba 25, 2019, yaliyofanyika Kitaifa
katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Mushi ametoa taarifa hiyo
katika Kilele cha Maadhimisho hayo, Oktoba 25, 2019 ambapo amebainisha
kuwa asilimia kubwa ya matatizo ya kisheria yalihusu migogoro ya ardhi
na yameshafikishwa mahakamani na yako katika hatua mbalimbali.
Amesema huduma walizopata wananchi
katika wiki ya msaada wa kisheria ni pamoja na huduma za usuluhishi,
ushauri wa kisheria, kuandaa nyaraka na maelekezo ya sehemu sahihi ya
kwenda pindi wanapopata migogoro.
“Mbali na huduma kwa wananchi
mafunzo yametolewa kwa makundi mbalimbali ya watumishi wa umma wapatao
1300 wakiwemo, wajumbe wa menejimenti ya sekretarieti ya mkoa, wajumbe
wa kamati ya parole, wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji,
wajumbe wa kamati ya maadili ya mahakimu, askari polisi na magereza,
wajumbe wa kamati za shule na watendaji wa vijiji na kata, “ alisema
Mushi.
Kwa upande wake Hakimu Mary
Nyangusi akimwakilisha Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Mary Mrio, ametoa wito kwa wananchi kuandika wosia ili
kupunguza migogoro ya ardhi ambayo mingi inatokea mara nyingi wanaume(
baba) wanapofariki na wake(mke) na watoto kudhulumiwa haki zao.
Adam Kisinza ni Mmoja wa wananchi
waliofika kupata msaada wa kisheria katika maadhimisho hayo amesema,
“nashukuru nimeelewesha ninachotakiwa kufanya maana kule kwetu baba
mwenye mji anapokuwa amefariki wakabaki watoto na mama, wanakuwa hawana
mamlaka juu ya mali iliyoachwa maana kila mtu anataka achukue chake
wakati mzee hakuacha hata wosia”.
Akifunga Maadhimisho ya Wiki ya
Msaada wa Kisheria,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni
vema wizara ya katiba na sheria ikaona umuhimu wa kupeleka maadhimisho
ya wiki ya msaada wa huduma za kisheria katika maeneo ambayo
hayajafikiwa na huduma hiyo, ili wananchi wapate uelewa wa masuala ya
kisheria na kupata matokeo yatakayoonekana.
Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa
Kisheria Kitaifa mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu:- “Msaada wa
Kisheria kwa Maendeleo Endelevu”ambapo kilele cha maadhimisho haya
kimeenda sambamba na uzinduzi wa Jarida la Msaada wa Kisheria, ambalo
limezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
0 comments:
Post a Comment