
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa kampuni ya kutengeneza
matrekta ya BTP , Alexsey Pankov (kushoto) na Ignat Dydyshko baada ya
mazungumzo kwenye hoteli ya Marriot ya Sochi nchini Urusi, Oktoba 22,
2019. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Mstaafu,
Simon Mumwi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiagana na Wakurugenzi wa kampuni ya kutengeneza matrekta ya BTP,
Alexsey Pankov (kushoto) na Ignat Dydyshko baada ya mazungumzo kwenye
hoteli ya Marriot ya Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Wakurugenzi wa kampuni ya kutengeneza matrekta ya BTP,
Alexsey Pankov (kuatikati) na Ignat Dydyshko kwenye hoteli ya Marriot ya
Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Russian Railways,
Alexander Misharin kabla ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Marriot ya
Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya ya
Zarubezhnefe, Bw. Sergey Kundryashov kwenye hoteli ya Marriot iliyopo
Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya ya
Zarubezhnefe, Bw. Sergey Kundryashov kwenye hoteli ya Marriot iliyopo
Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Russian
Railways, Bw. Alexander Misharin na kumweleza kuwa Tanzania inahitaji
sana kuimarisha usafiri wa ndani wa reli hasa katika Majiji ya Dar es
salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na Tanga.
Amesema kampuni hiyo yenye
uwezo mkubwa wa kujenga reli mpya, kukarabati reli, kutengeneza injini
za treni na mabehewa pamoja na ukarabati wake inahitajika sana nchini
ili kufanikisha mpango wa Serikali wa kuimarisha reli za zamani za
TAZARA, Reli ya Kati na kufugua reli ya Kaskazini inayounganisha mikoa
ya Dar es salaam, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
Waziri Mkuu alizungumza na
Mkurugenzi huo jana (Oktoba 22, 2019) kwenye hoteli ya Marriot iliyopo
Sochi nchini Urusi, ambapo alitumia fursa hiyo kuikaribisha kampuni ya
Russian Railways kuwekeza nchini hususani katika sekta ya ujenzi, ufundi
na mafunzo ikishirikiana na makampuni ya Watanzania.
Waziri Mkuu yuko nchini Urusi
kuhudhuria mkutano baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa ya
Afrika na Urusi (Russia-Africa Summit), unaotarajiwa kuanza leo Oktoba
23 hadi 24, 2019 katika jiji la Sochi. Waziri Mkuu anahudhuria mkutano
huo kwa niaba ya Rais, Dk. John Pombe Magufuli.
“Katika kipindi hiki ambacho
Tanzania inajenga reli ya kiwango cha kimataifa ya SGR pamoja na kufufua
reli ya Kaskazini, inaikaribisha Kampuni ya Russian Railways kwa mikono
miwili ije ifanye mazungumzo rasmi na Wizara husika. Pia Serikali inao
mkakati wa kujenga reli mpya katika ukanda wa Kusini kutoka Mtwara hadi
Ruvuma ili kuiunganisha bandari ya Mtwara na mikoa ya Kusini pamoja
na nchi jirani za Malawi na Zambia.”
Alisema Tanzania kwa sasa
inahitaji sana kuimarisha usafiri wa ndani wa reli hasa katika majiji ya
Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na Tanga hivyo endapo
mazungumzo kati ya Wizara husika na kampuni hiyo yataonekana kuwa na
tija na yana maslahi kwa Watanzania, kampuniyo itapewa fursa ya kuwekeza
nchini.
Kadhalika, Waziri Mkuu
alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wafanyabiashara wa Tanzania, wito wa
Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kuwataka watumie fursa lukuki zilizopo
nchini kuanzisha makapuni ya pamoja na makampuni ya nje ili kuunganisha
nguvu kwa kuendesha kwa pamoja makampuni yatakayoanzishwa.
Alisema utaratibu wa makampuni
ya Tanzania kuanzisha makampuni ya pamoja na makampuni ya nje utawapa
Watanzania fursa ya kujipatia kipato pia wataweza kulinda maslahi ya
Taifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mkuu wa Kapuni ya Russia Railways, Bw. Misharin alimuhakikishia Waziri
Mkuu kuwa kampuni yake iko tayari kushirikiana na wafanyabiashara wa
Kitanzania katika kuanzisha makapuni ya pamoja ili kuipatia Tanzania
tekinolojia ya masuala ya reli na kubadilisha ujuzi.
Awali, Waziri Mkuu alizungumza
na Wakurugenzi wa Kampuni ya kutengeneza matrekta ya BTP, Bw. Alexsey
Punkov na Bw. Ignat Dydyshkoa ambaye alisema kuwa kampuni
yake inakusudia kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya kilimo kwa
kuleta nchini mashine mbalimbali kama vile matrekta na mitambo ya
ujenzi wa barabara.
Viongozi wote wa makampuni ya
Urusi waliozungumza na Waziri Mkuu waliahidi kuja Tanzania mwaka huu
ili kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji na kufanya mazungumzo yenye
lengo la kushirikiana na wafanyabiashara wa Kitanzania katika uwekezaji
wao wanaokusudia kuufanya nchini.
Mheshimiwa Majaliwa pia
alizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya
Zarubezhnefe, Bw. Sergey Kundryashov ambaye pia alionyesha nia ya kutaka
kuwekeza nchini Tanzania.
Katika safari hiyo Waziri Mkuu
ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya
Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja
Jenerali Mstaafu, Simon Mumwi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo
ya Petroli Tanzania (TPDC), James Matarajio.
0 comments:
Post a Comment