
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Halamashauri ya Wilaya ya Moshi Kastori Msigala baada ya
kukagua Majalada ya Ardhi katika Ofisi za Ardhi za Halamashauri hiyo
jana wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta hiyo mkoani
Kilimanjaro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Kastori Msigala kabla ya
kuondoka jana wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta
hiyo mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi
Warioba.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua maendeleo ya ujenzi wa
Ofisi na Nyumba za Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) katika shamba la
Miti la Kilimanjaro Kaskazini (Rongai) uliopo wilayani Rombo mkoa wa
Kilimanjaro jana wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo. Kulia
ni Mhandisi wa ujenzi wa mradi huo kutoka Shirika la Nyumba la Taifa
Peter Mwaisabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akioongozwa na Kaimu Meneja wa
Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Kilimanjaro Stanley Msoffe (Kulia)
kwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Wakala wa
Huduma za Misitu (TFS) katika shamba la miti la Kilimanjaro Kaskazini
(Rongai) uliopo wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro jana wakati wa ziara
yake ya siku mbili mkoani humo.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wafanyakazi
wanaojenga nyumba za watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS) katika shamba la miti la Kilimanjaro Kaskazini (Rongai) lililopo
Rombo mkoa wa Kilimanjaro wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi
na Nyumba za TFS jana wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
…………………….
Na Munir Shemweta, WANMM KILIMANJARO
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameziwataka idara za ardhi
katika halmashauri nchini kuyabainia mashamba yote yasiyoendelezwa
(Mashamba Pori) na kupeleka mapendekezo ya kufutwa mashamba hayo
Wizarani.
Dkt Mabula alisema hayo jana
alipokutana na watendaji wa sekta ya ardhi pamoja na wakurugenzi wa
halamashauri zote za mkoa wa Kilimanajaro akiwa katika zaiara yake ya
siku mbili mkoani humo kukagaua utendaji kazi wa sekta ya adhi.
Dkt Mabula alisema, pamoja na
baadhi ya mashamba kufutwa katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na
kutoendelezwa lakini kuna maeneo mengine maafisa ardhi wameshindwa
kuyatolea taarifa mashamba yasiyoendelezwa ili yafutwe kwa sababu
wanazozijua wenyewe.
‘’Nataka taarifa ya mashamba
yote pori katika halmashauri yabainishwe na kutolewa taarifa ili tuweze
kupeleka mapendekezo ya kufutwa mashamba hayo kwa rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania’’ alisema Dkt Mabula
Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, taarifa ya kubaini mashamba yote
pori katika kila halmashauri ziwe zimewasilishwa kufikia desemba mwaka
huu na Januari 2010 timu maalum itaundwa kwa ajili ya kazi hiyo.
Dkt Mabula alisema, Afisa
Ardhi katika halmashauri yoyote atakayebainika kuficha ukweli kuhusiana
na uwepo mashamba pori katika eneo lake hatua kali za kinidhamu
zitachukuliwa dhidi yake.
‘’Maafisa Ardhi mnashirikiana
na baadhi ya wenye mashamba pori na mnashindwa kuleta mapendekezo ya
kufutwa mashamba, sisi tunahitaji kuona kila ardhi inatumika katika
malengo yaliyokusudiwa’’ alisema Dkt Mabula
Mapema katika kikao hicho,
baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Kilimanajaro pamoja na
Maafisa Ardhi alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi kuwa, idara za ardhi katika halmashauri zao zinakabiliwa na
changamoto kubwa za upungufu wa watumishi katika fani tofauti za sekta
ya ardhi pamoja na bajeti finyu.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Moshi Kastori Msigala alieleza kuwa halmashauri
yake inakabiliwa na upungufu wa watumishi katika fani za Mipango Miji,
Upimaji na Uthamini jambo alilolieleza kuwa linachangia kwa kiasi
kikubwa kutofikia malengo katika sekta ya ardhi.
Katika hatua Nyingine Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Wakala wa
Huduma za Misitu TFS katika Shamba la Miti la Kilimanjaro Kaskazini
maarufu kama Rongai lililopo wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro
Kwa mujibu wa Kaimu Meneja wa
Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Kilimanjaro Stanley Msoffe, Ujenzi
wa Ofisi na Nyumba za Watumishi wa TFS unaofanywa na NHC unagharimu
zaidi ya milioni 532.9 unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2020
0 comments:
Post a Comment