METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, October 3, 2019

Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V Umefanya Mkutano Mkuu na kuchagua Viongozi



Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V umefanya  mkutano mkuu wa uchaguzi mjini Aschaffenburg Ujerumani jumamosi 28.09.19.  Katika uchaguzi huo watanzania wanaoishi ujerumani walichagua viongozi wapya, nafasi ya mwenyekiti alichaguliwa Mwl. Bi Upendo Vanessa Lyimo Foelesen kuwa mwenyekiti wa UTU e.V,  baada ya mwenyekiti mstaafu Bw. Mfundo Peter Mfundo kukataa kugombea nafasi hio, ambayo amekaa kwa muda wa miaka 9, na kukitumikia chama hicho kwa muda wote huo, hata hivyo kamati ilimuomba achukue nafasi ya heshima kuwa mwanakamati, mshauri, mlezi wa UTU e.V na kiongozi muandamizi katika shughuli za UTU e.V
 Watanzania wanaoishi ujerumani waliwachagua  viongozi wafuatao.
 Mwenyekiti: Mwl. Bi Upendo Vanessa Lymo
Makamo Mwenyekiti:  Bw. Malumbo Salim Malumbo 
Katibu:  Bi.  Petrida Karch
Muweka hazina: Bw. Mngoya Lukuta
Wanakamati:
Bw. Mfundo Peter Mfundo  
Bw. Ebrahim Makunja (aka Kamanda Ras Makunja)
Bw. Sudi Mnette
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com