![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/1-2.png)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/1b.png)
Mtambo/Rigi inayotumika katika Ucchorongaji wa Visima vifupi vya utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi wembere.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/2.png)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/2b.png)
Wachimbaji (drillers) kutoka
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambao ndio wamepewa kandarasi ya
kuchimba visima vya utafiti katika Bonde la Wembere wakiendelea na kazi.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/3.png)
Wataalamu wa masuala ya miamba
kutoka TPDC wakiangalia baadhi ya Sampuli za Utafiti wa Mafuta katika
Bonde la Eyasi Wembere. Sampuli hizi zinazopatikana katika kila hatua ya
uchimbaji unavyoendelea
…………………..
Igunga,Tabora
Serikali kupitia Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imeanza kufanya utafiti wa mafuta
ya petroli katika bonde la Eyasi Wembere, Utafiti huu unahusisha
uchorongaji wa visima vitatu vya utafiti vyenye urefu wa mita 300 kila
kimoja na hivyo kufanya jumla ya mita 900 zitakazochorongwa katika Bonde
la Eyasi Wembere ambapo Kisima namba moja kinachorongwa katika Kijiji
cha Kining’nila Wilaya ya Igunga,kisima namba 2 na 3 vitachoroongwa
katika wilaya za Meatu Mkoani Simiyu na Iramba Mkoani Singida.
Akiongea na waandishi wa habari
wakati wa uzinduzi rasmi wa uchorongaji wa kisima namba 1, Meneja
utafutaji wa Mafuta na Gesi kutoka TPDC, Bi Venosa Ngowi alisema kuwa
utafiti huu unakuja kufuatia ukusanyaji taarifa za bonde hilo
uliofanyika mwaka 2015 kwa kutumia ndege maalumu. Bi Ngowi alisema baada
ya utafiti huo wa kutumia ndege, ulionesha eneo la Bonde la Eyasi
Wembere kuwa na miamba tabaka mizuri ambayo inaweza kutumika kwaajili ya
utafiti wa Mafuta na gesi hivyo uchorogaji huu wa visima vifupi vya
utafiti ni awamu ya pili kufuatia utafiti wa 2015/16.
Bi Ngowi aliendelea kwa kusema
kwamba eneo lote la Bonde la Eyasi Wembere ni muhimu kwaajili ya utafiti
huo kutokana na aina ya miamba inayopatikana. Akizunguzmia mita
zilizochorongwa Katika kisima namba 1 kilichoanza kuchorongwa katika
Wilaya ya Igunga amesema tayari zimechoronga mita 116 kati ya 300
zinazopaswa kuchorongwa.
Nae Meneja Mradi wa Utafutaji
Mafuta katika bonde la Eyasi Wembere, ndugu Sindi Mduhu alisema eneo la
Bonde la Eyasi Wembere ni kubwa na linaanzia katika Mikoa ya Manyara,
Singida,Simiyu, Tabora pamoja na Arusha. Baada ya ukusanyaji takwimu za
eneoo hilo, kilichofanyika ilikuwa ni kuzichakata na kuzitafsiri ili
kuweza kuona ni wapi palio na miamba tabaka yenye kina kirefu ambacho
kianweza kutunza mafuta. “Kijiji cha Kining’inila ni mojawapo ya eneo
ambalo lilanishwa kama moja ya eneo ambalo uchoroongaji wa visima
unaweza kufanyika”.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa TPDC, Dkt James Mataragio aliyefika ene la utafiti kwaajili
ya kujionea kinachoendelea katika utafiti huo alisema utafiti huo
unafanyika kwa matumaini kuwa Tanzania inaweza kugundua mafuta.
“Tunafanya Utafiti kwa kutegemea kwamba kwa kipindi kisichozidi miaka
mitano (5) huenda tukagundua mafuta na hivo leo nawadhibitishia
watanzania kwamba kazi hiyo inaendelea”. Dkt. Mataragio aliendelea kwa
kusema “ kama kule Uganda huenda tukawa na mafuta”.
Uchorongaji huo utafuatiwa na ukusanyaji wa taarifa za mitetemo ili kuonesha maeneo ambayo yanaweza kuwa na mafuta.
Dkt.mataragio aliongeza kwa kusema
kuwa ni nia ya dhati ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha kwamba TPDC si kwamba tu inachimba
gesi yake yenyewe bila pia kuhakikisha inagundua mafuta. “ Mhe. Rais
angependa kwamba katika kipindi ambacho atakuwa madarakani tuwe
tumekwishagundua mafuta kwani tayari tunayo gesi asilia ambayo kwa mwaka
2020 tutaongeza visima vingine ambavyo tutavifanya wenyewe TPDC na sio
kwa kutumia wawekezaji kutoka nje ya nchi”.
Kwa upande wa ushirikishaji
makampuni ya ndani katika utafiti huo, Dkt Mataragio alisema kazi yote
inafanywa na TPDC kwa kushhirikiana na STAMICO ambalo ni shirika la
Serikali na ndiye Mkandarasi Mkuu katika mradi huo.
Akitaja sifa za maeneo ambayo
mafuta yanaweza kugundulika, Dkt.Mataragio alisema ni maeneo ya Bonde la
Ufa ambapo kama ilivyo kule nchini Kenya katika eneo la Lokcha au
Turkana lipo katika Bonde la Ufa na kule wamegundua mafuta. Vile vile
ukienda Uganda Ziwa Albert ambalo lipo katika Bonde la Ufa nao vile vile
wamegundua mafuta. Kwa upande wa Tanzania, katika eneo la Ziwa
Tanganyika ambalo lipo katika Bonde la ufa kuna matonetone ya mafuta
hivyo ni dalili nzuri ya uwezekano wa upatikanaji wa mafuta na tayari
ukusanyaji wa taarifa za eneo hilo ulikwishafanyika hivyo
kitakachofuatia ni ufuatiliaji.
Dkt. Mataragio aliongeza kwa
kutaja gharama za mradi wa uchoorgaji visima hivyo mbapo kwa visima
vyote vitatu hadi vikamilike vitagharimu fedha za Kitanzania shilingi
milioni mia tatu ambapo katika utafiti wa ndege jumla ya shlingi za
Kitanzania shilingi bilioni mbili nukta nne (2.4) zote zikiwa ni fedha
za ndani na Serikali.
Mwenyekiti wa Kijiji cha
Kining’inila Christopher Njilezengo ambapo ndipo utafiti huo unafanyika,
aliipongeza Serikali kwa kukubali kuwekeza katika mradi huo kwani
utakuwa na tija kwa taifa endapo utafanikisha upatikanaji wa mafuta.
“Tunaishukuru sana Serikali kupitia TPDC kwani tunaamini ya kwamba
wanatekeela sera ya chama cha mapinduzi chini ya uongozi shupavu wa Mhe.
Rais Magufuli ambapo asingekuwa yeye basi mambo hayo wasingeyaona”.
Bi. Neema Masanja mkazi wa Kijiji
cha Kining’inila ambapo ndipo utaifit uanfanyika aliiipongeza Serikali
kwa utafiti huo na kunonesha matumaini makubwa katika utafiti
unaofanyika na endapo mafuta yatapatikna. “ Mafuta yakipatikana
itawezesha upatikanaji wa fursa mbalimbali kwa wanachi ili kuleta
maendeleo katika Kijiji chetu na taifa”.
Tayri baadhi ya wanachi wa Kijiji
hicho wameanza kuonja neema ya utafiti huo ambao kuna baadhi yao
wamepatiwa kazi mbali mbali zisizohitaji elimu kubwa kama vile upishi,
ulinzi pamoja na vibarua.
0 comments:
Post a Comment