Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa sekta ya ardhi wa wilaya
ya Mkuranga mkoani Pwana jana alipofanya ziara ya kuhamasisha ukusanyaji
kodi ya ardhi na kutatua migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo. Kulia ni
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Philberto Ngasa.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa sekta ya ardhi wa wilaya
ya Mkuranga mkoani Pwana jana alipofanya ziara ya kuhamasisha ukusanyaji
kodi ya ardhi na kutatua migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo. Kulia ni
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Philberto Ngasa.
………………….
Na Munir Shemweta, WANMM MKURANGA
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
amepiga marufuku utoaji vibali vya ujenzi wa viwanda katika maeneo ya
makazi ya watu katika wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Dkt
Mabula alitoa kauli hiyo jana tarehe 03 Oktoba 2019 alipokutana na
uongozi pamoja na watumishi wa sekta ya ardhi wakati wa ziara yake ya
siku moja wilayani Mkuranga mkoani Pwani kuhamasisha ukusanyaji maduhuli
ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kutatua migogoro ya ardhi.
Alisema,
halmashauri ya wilaya ya Mkuranga lazima iandae Mpango Kabambe
alioueleza kuwa utakuwa dira ya halmashauri hiyo kuonesha matumizi ya
ardhi yake kwa kuwa maeneo kama viwanda, makazi na matumizi mengine
yatakuwa yameoneshwa na kuondoa ujenzi wa makazi holela.
‘’Mkuranga
lazima iwe na mpango wa matumizi ya ardhi unaoonesha viwanda vikae
wapi, siyo viwanda kujengwa kila kona na katika mipango yenu halmashauri
muandae maeneo yatakayowekwa viwanda’’ alisema Dkt Mabula.
Kuhusu zoezi la Urasimishaji, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameitaka
Mkuranga kuharakisha zoezi hilo ili kuepuka makazi holela na kubainisha
ucheleweshaji wowote utasababisha mji kutopangika na kusisitiza zoezi
hilo lazima lisimamiwe kwa umakini.
Akigeukia
suala la upimaji maeneo katika wilaya ya Mkuranga, Dkt Mabula alisema
wilaya ya Mkuranga bado hajafanikiwa katika zoezi la upimaji pamoja na
kuwa na viwanda vingi na kushauri wakati wa zoezi la upimaji lazima
halmashauri iainishe pia maeneo ya uwekezaji,
Kwa
upande wake Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega alisema, wilaya ya Mkuranga ina viwanda
vingi kutokana kuwa na eneo linalovutia na kuongeza kuwa atafurahi kama
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi itafanya jitihada za
kuharakisha zoezi la urasimishaji.
‘’Kama
serikali itaongeza kasi kidogo ya kupanga na kurasimisha maeneo ya
wilaya hii basi itakusanya kiasi kikubwa cha fedha maana Mkuranga
imekuwa lango la ni kimbilio la wananchi kutoka Dar es Salaam kutokana
na mkoa huo kujaa na mahali pekee pa kupumulia ni Mkuranga’’ alisema
Ulega.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Mhandisi
Mshamu Munde alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi kuwa halmashauri yake ina
migogoro mingi ya adhi ya kurithi na katika kukabiliana changamoto za
ardhi ikiwemo makazi holela, tayari kuna Kampuni saba zinazofanya kazi
ya urasimishaji na kusisitiza kuwa mkakati wa halmashauri yake ni kuzuia
uanzishwaji makazi holela,
Katika hatua nyingine
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Philberto Sanga amemtaka mtumishi wa sekta
ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Welbert Mduma
kujisalimisha mara moja wilayani humo kujibu tuhuma zinazomkabili za
kuhujumu mradi wa upimaji viwanja vya halmashauri ya wilaya ya Mkuranga
katika maeneo ya Kikoo na Miale.
Mtumishi
huyo ambaye ni Afisa Ardhi hajaonekana ofisi za halmashauri ya wilaya
ya Mkuranga kwa muda mrefu tangu arejeshwe akitokea Morogoro
alipohamishiwa baada ya kufanya ‘madudu’ katika mradi wa fidia ya ardhi
katika maeneo yaliyopimwa viwanja na halmashauri ya Mkuranga.
0 comments:
Post a Comment