Mkurugenzi Msaidizi -Masoko ya mazao Wizara ya Kilimo Benito Kavenuka
akitoa salamu za wizara wakati wa ufunguzi wa mkutano maalum wa Jumuiya ya
Wasindikaji Nafaka nchini.Mkutano huu umefanyika leo Jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na wasindikaji nafaka toka mikoa yote.
Mwenyekiti wa muda wa Jumuiya ya Wasindikaji Nafaka ( JUWANATA) Oscar
Munisi akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano maalum wa katiba wa jumuiya hiyo
jijini Dar es Salaam .Lengo la mkutano huo ni kupitisha katiba itakayoongoza
wasindikaji nafaka nchini katika kutafuta suluhisho la masoko ya bidhaa.
Mjumbe wa kamati ya Juwanata Aminiel Maro akisoma rasimu ya Katiba ya
umoja huo,wakati wa mkutano maalum kujadili na kupitisha katiba hiyo kwa
wajumbe leo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wajumbe wa mkutano maalum wa kupitisha katiba ya kuanzisha
Jumuiya yawasindikaji nafaka nchini wakifuatilia mada za mkutano leo jijini Dar
es Salaam.
Na
Revocatus Kassimba, Dar es Salaam
Serikali
imeupongeza uongozi wa muda wa Jumuiya ya Wasindikaji Nafaka Tanzania
(JUWANATA) kwa kukamilisha rasimu ya katiba ya umoja wao.
Pongezi
hizo za serikali zimetolewa leo na Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Masoko
toka Wizara ya Kilimo Benito Kavenuka wakati wa mkutano maalum wa Juwanata
uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kavenuke
amesema kuundwa kwa jumuiya ya wasindikaji mazao ya nafaka ni utekelezaji wa
azimio la mkutano wa wafanyabiashara ya mazao ya nafaka uliofanyika mwezi Agosti
mwaka huu chini ya Waziri wa Kilimo.
“Serikali
inaunga mkono Juwanata kwa kutekeleza kwa haraka azimio la mkutano wa Waziri wa
Kilimo na wafanyabiashara wa nafaka la kuanzisha jumuiya hii muhimu kwa ustawi wa viwanda vya mazao ya nafaka.”
alisema Kavenuka.
Aliongeza
kusema serikali itapenda kuona Viongozi wa jumuiya hii wanasimamia viwango vya
ubora wa bidhaa za nafaka zinazalishwa
ili kuwa na uhakika wa soko na bei nzuri.
Kavenuka
amewataka pia kuongeza wigo wa kuwafikia wasindikaji waliopo mikoani kujiunga
na jumuiya hii,ili serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo iwe rahisi
kutoa huduma za kukuza sekta ya usindikaji nafaka nchini.
Akitoa
taarifa ya mkutano huo maalum,Mwenyekiti wa muda wa Juwanata Oscar Munisi
alisema lengo la jumuiya ni kuitikia kwa
vitendo kauli mbiu ya serikali ya kujenga viwanda vya kuongeza thamani mazao ya
nafaka.
Munisi aliongeza kusema jumuiya yao inaundwa
na wanachama wamiliki wa viwanda vya kusindika nafaka na mafuta toka mikoa yote
ya Tanzania bara ambapo kazi ya kuandaa katiba ya muda ilishirikisha wadau wote
“Tunataka
kuwa na Katiba itakayosaidia kusajili wasindikaji wote nchini hususan
wajasiliamali wadogo ili tuwe na sauti ya pamoja katika kuyafikia masoko ya
bidhaa za nafaka kwa ushirikiano na serikali” alisema Munisi
Alitaja
changamoto ya wajasiliamali wasindikaji kwa
sasa nchini kuwa ni kufikia masoko kama ya Lubumbashi Kongo imekuwa ngumu kwa kukosekana
chombo cha kuwaratibu.
Kwa
upande wake Meneja Mradi wa Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki (EAGC) Ikunda
Terry amewataka wasindikaji hususan wa mchele
kuongeza ubora ili kufikia soko
kubwa la nchi za Uarabuni.
“Tanzania
ina fursa ya soko la uhakika la mchele kwani sasa uzalishaji umefikia tani 2,200,000 wakati matumizi ya ndani kwa mwaka ni kama tani milioni moja,kwa
hiyo tunayo ziada ya zaidi ya tani milioni moja kwa ajili ya kuuza nje ya nchi” alisisitiza Ikunda.
Kufanyika
kwa mkutano huu maalum kunafatia mkutano wa Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga
alioitisha hapo tarehe 29 na 30 Agosti mwaka huu kujadili changamoto za masoko
ya mazao ya nafaka nchini.
0 comments:
Post a Comment