Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.
Binilith Mahenge,akizungumza na wadau wakati wa ufunguzi wa Mkutano
Baina ya Tanesco na Wateja wakubwa wa kanda ya kati wenye lengo ya
kuimarisha Sekta ya Nishati Nchini uliofanyika jijini Dodoma leo.
Meneja Mwandamizi Tanesco kanda ya
kati Mhandisi Atanas Nangali,akisoma Hotuba kwa mgeni rasmi Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge wakati wa ufunguzi wa Mkutano Baina
ya Tanesco na Wateja wakubwa wa kanda ya kati wenye lengo ya kuimarisha
Sekta ya Nishati Nchini
Sehemu ya wadau wakimsikiliza Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (hayupo pichani ) wakati wa
ufunguzi wa Mkutano Baina ya Tanesco na Wateja wakubwa wa kanda ya kati
wenye lengo ya kuimarisha Sekta ya Nishati Nchini uliofanyika jijini
Dodoma leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.
Binilith Mahenge,akisisitiza jambo kwa washiriki (hawapo pichani) wakati
wa ufunguzi wa Mkutano Baina ya Tanesco na Wateja wakubwa wa kanda ya
kati wenye lengo ya kuimarisha Sekta ya Nishati Nchini uliofanyika
jijini Dodoma leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.
Binilith Mahenge,akimsikiliza Meneja Mwandamizi Tanesco kanda ya kati
Mhandisi Atanas Nangali,mara baada ya kufungua Mkutano Baina ya Tanesco
na Wateja wakubwa wa kanda ya kati wenye lengo ya kuimarisha Sekta ya
Nishati Nchini uliofanyika jijini Dodoma leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.
Binilith Mahenge,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua
Mkutano Baina ya Tanesco na Wateja wakubwa wa kanda ya kati wenye lengo
ya kuimarisha Sekta ya Nishati Nchini uliofanyika jijini Dodoma leo.
………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKUU wa MkOA wa
Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amelitaka Shirika la Umeme nchini (TANESCO)
Kanda ya kati kuanzisha kitengo cha huduma ya haraka (fastruck) ili
kuondoa vikwazo kwa wawekezaji kupata huduma hiyo.
Agizo hilo amelitoa
leo jijini Dodoma wakati wa mkutano wa kujadili changamoto mbalimbali
baina ya TANESCO,wawekezaji na wenye viwanda kutoka mikoa ya Kanda ya
kati,wenye lengo la kuimarisha sekta ya Nishati Nchini
Dkt Mahenge amesema
kuwa pamoja na kuwa Sera zipo wakati mwingine mnapaswa kwenda nje ya
box kubuni utaratibu ambao unawawezesha wawekezaji kupata kwa haraka
huduma za Umeme ili walete tija katika mkoa na taifa kwa ujumla hasa
ukizingatia tunaelekea katika uchumi wa kati wa viwanda.
“Naomba ifike wakati
muwe mnaenda nje ya box,lengo ni kujenga wala sio kubomoa,hivyo ni vema
kuwapa kipaumbele wawekezaji ili waanze kutoa huduma ya uwekezaji wa
viwanda kwa haraka,” amesema Dkt Mahenge.
Aidha Dkt.Mahenge
amelitaka Shirika la Tanesco kuboresha huduma za Umeme katika maeneo ya
Mpwapwa,Kongwa,Kibaigwa,Narco,Bahi na Chemba ili iwe rahisi wawekezaji
kwenda kuwekeza katika maeneo hayo.
”Mkifanya hivyo
katika maeneo hayo ambayo yamekuwa yanaleta shida ya umeme mtakuwa
mmesaidia kutatua changamoto za wakazi wa maeneo hayo na wawekezaji”
amesisitiza Dkt.Mahenge
Hata hivyo Dkt.Mahenge amewapongeza Tanesco mkoa wa Dodoma kutokana na maboresho ya upatikanaji wa umeme yanayofanyika.
Awali Meneja wa
TANESCO Kanda ya Kati Mhandisi Atanas Nangali amesema kuwa
wamelazimika kuitisha kikao hicho ili kuangalia njia bora ya kuboresha
huduma na kufahamu changamoto zinazowakabili katika kulipa madeni,lakini
kubwa zaidi ni kuboresha uhusiano.
“Historia ya Shirika
letu inaonyesha wenye viwanda na wawekezaji wote wakubwa wamekuwa
wakichangia zaidi ya asilimia 50 ya pato la Shirika hivyo kikao hiki ni
muhimu kuangalia bora ya kuboresha mahusiano kati yetu na wateja,”
amesema Nangali.
Hata hivyo Mhandisi
Nangali,amesema kuwa katika kuboresha miundombinu Tanesco Kanda ya kati
inayohudumia mikoa ya Morogoro,Singida na Dodoma imeanza kufanya
utanuzi wa kituo cha kupoza Umeme cha Dodoma kutoka uwezo wa sasa
Megawati 48 hadi kufikia Megawati 400.
Mhandisi Nangali
amesema kuwa miradi mingine ni kituo kipya cha kupiga Umeme kilichopo
Ifakara mkoani Morogoro, ambacho kutakuwa na uwezo wa kuzalisha
Megawatts 16 na kituo kile cha singida kitakachoongezewa uwezo kutoka
megawatts 32 hadi 400.
0 comments:
Post a Comment