Jengo la kituo cha umahiri lililopo Musoma
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo mbele katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Viomgozi wa
Serikali, Wizara ya Madini pamoja na Wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Mara
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo kushoto, anaefata ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya
MadiniIssa Nchasi wakikabidhiwa funguo ya jengo la Umahiri na Meneja wa
SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni Fabian Buberwa
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo mbele katikati akifanya ukaguzi wa jengo la umahiri kabla ya
makabidhiano, mbele kulia ni Meneja wa SUMA JKT Kanda ya ziwa Kapteni
Fabian Buberwa, kushoto ni kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara
Samwel Mayuki, nyuma kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vicent
Naano, nyuma kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya
Madini Issa Nchasi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara
Caroline Mthapula akitoa maelezo juu ya sekta ya madini Mara, kutoka
kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini. Issa Nchasi,
anaefata ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, na kushoto ni
Meneja wa SUMA JKT Kanda ya ziwa Kapteni Fabian Buberwa
Kaimu Meneja wa Mradi wa Usimamizi
Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Veronica Francis akiwakirisha
taarifa za Kituo cha umahiri cha Musoma
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi akitoa taarifa za kukamilika kwa jengo la kituo cha umahiri Mara
8Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mara
………………..
Na Tito Mselem, Musoma
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo leo Oktaba 07, 2019 amekabidhiwa jengo lenye thamani ya shilingi
bilioni 1.2 ambalo litatumika kama kituo cha umahiri kwa wachimbaji
wadogo wa Madini Mkoani Mara.
Jengo hilo lililojengwa na
Mkandalasi SUMA JKT na kukabidhiwa kwa Wizara ya Madini kupitia Naibu
Waziri Nyongo,nae pia kalikabidhi jengo hilo kwa Tume ya Madini ambapo
limekamilika na likotayari kwaajili ya matumizi.
Aidha Jengo hilo la umahiri ni
kati ya majengo saba ya umahiri na jengo moja la taaluma lililopo Chuo
cha Madini Dodoma (MRI) yaliyojengwa kwa jumla ya thamani ya Bilioni
11.9na SUMA JKT kupitia mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini
(SMMRP) ambayo yamejengwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo
Kagera, Musoma, Bariadi, Chunya, Mpanda, Handeni Tanga na Songea.
Akizungumza kwenye
makabidhiano hayo Naibu Waziri Nyongo ameipongeza SUMA JKT kwa kazi
nzuri waliyoifanya ya ujenzi wa jengo hilo ambalo limekamika kwa wakati.
Naibu Waziri Nyongo amesema
lengo kuu la kuanzisha vituo hivyo ni kuwasadia wachimbaji wadogo
kufanya shughuli za madini kwa tija kwa kuwapatia elimu ya uchimbaji
katika vituo hivyo.
“faida ya ujenzi huu ni kutoa
mafunzo ya kitaalamu yahusuyo Madini, tutatoa mafunzo ya Utafiti wa
Madini, ikiwa ni pamoja na kuonesha mikanda ya Madini ilipo na muelekeo
wake, uchimbaji wa madini wenye tija na salama, Uchenjuaji wenye kuleta
uvunaji mkubwa wa madini na hivyo kuwapatia faida kubwa wachimbaji”,
alisema Nyongo.
Inakadiliwa kuwa baada ya
mafunzo kupatiwa kwenye vituo hivi, wachimbaji watavuna madini kwa zaidi
ya asilimia 80ukilinganisha na hapo awali ambapo wachimbaji wengi
walivuna dhahabu kwa asilimia 30 tu,
Imeelezwa kuwa katika vituo
hivi vya umahiri kutakuwa na mafunzo ya kuomba leseni kwa njia ya
mtandao na kutakuwa na usagaji wa mawe na kupima sampuli mbalimbali za
madini.
Aidha Nyongo ametoa rai kwa
wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Mara wakitumie kituo hicho cha umahiri ili
viwaletee tija na faidsa katika shughuri za uzalishaji madini.
Kwa upande wake kaimu meneja
wa mradi wa usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Veronica
Francis alisema kuwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST)
ulifanya utafiti wa kijiolojia na kubaini maeneo saba nchini kwa ajili
ya ujenzi wa vituo vya umahiri.
“Utafiti umebaini kuwepo kwa
kiwango kikubwa cha dhahabu katika eneo la Buhemba yenye takribani wakia
10,737 zenye viwango vya 0.7g/t ndiyo maana kituo hiki kikaja kujengwa
hapa Musoma ili kiwasaidie wachimbaji wadogo kupata mafunzo ya namna
bora ya uchimbaji madini,” alisema Veronika.
Pia Mkuu wa Wilaya ya Musoma
Dkt. Vicent Naano ameipongeza Wizara ya Madini kwa Kujenga kituo cha
umahiri katika Mkoa wa Mara maana kitawasaidia sana wachimbaji kufanya
kazi kwa uhakika na sio kubahatisha.
0 comments:
Post a Comment