
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela akichora mstari wa mahudhurio ya waalimu wa Shule ya
Msingi Iyula Wilaya ya Mbozi ikiwa ni saa nne asubuhi mara baada ya
kubaini kuwa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo hachori mstari ifikapo saa 1:45
asubuhi ili kuwabaini wachelewaji.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela akikagua daftari la mahudhurio ya waalimu wa Shule ya
Sekondari Simbega iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi na kubaini
utoro na uchelewaji wa waalimu katika shule hiyo.
…………………..
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela amefanya ziara ya kushtukiza katika baadhi ya shule
za Msingi na Sekondari na kisha kumuagiza Afisa Elimu Mkoa kuwachukulia
hatua za kinidhamu waalimu wote ambao wanachelewa au kutohudhuria
shuleni.
Brig. Jen. Mwangela ametoa agizo
hilo mapema leo mara baada ya kutembelea shule za sekondari za Myovizi
na Simbega pamoja na Shule ya Msingi Iyula za Halmashauri ya Wilaya ya
Mbozi na kubaini utoro na uchelewaji wa waalimu mara baada ya kukagua
madaftari ya mahudhurio.
“Mahudhurio ya waalimu sio mazuri,
waalimu hawafiki wote katika shule zao na wengine huchelewa sana, pia
vitabu vya mahudhurio havijafungwa ifikapo saa moja na nusu na saa moja
na dakika 45 kama inavyotakiwa ili kuwabana wachelewaji.”, amesema Brig.
Jen. Mwangela.
Brig. Jen. Mwangela amesema Afisa
Elimu Mkoa anapaswa kusimamia mahudhurio ya waalimu kwakuwa msingi wa
taifa unajengwa shuleni na msingi huo hauta imarika endapo waalimu
watakosa nidhamu katika kuwahi na kuhudhuria shuleni.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya
Sekondari Myovizi Tabu Mtafya amesema amekuwa akitoa onyo kwa waalimu
ambao wanachelewa hivyo agizo la Mkuu wa Mkoa ataendelea kulitekeleza.
“Baada ya Mkuu wetu wa Mkoa
kukagua kitabu cha Mahudhurio ameniagiza niendelee kusimamia mahudhurio
ya waalimu, nami nitawaita waalimu wote wa shule yangu niwakumbushe juu
ya kuwahi na kutimiza wajibu wao.”, amesema Mtafya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John
Palingo amekiri kuwepo kwa mapungufu ya waalimu kutohudhuria au
kuchelewa shuleni na hivyo wamejipanga katika Wilaya ya hiyo kusimamia
mahudhurio ya waalimu na kwachukulia hatua za kinidhamu waalimu watoro
na wachelewaji.
0 comments:
Post a Comment