
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji,
Mhandisi Anthony Sanga (aliyekaa kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA),
Mhandisi Leonard Msenyele (kushoto) wakisaini nyaraka za makabidhiano ya
Ofisi. Awali Mhandisi Sanga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji MWAUWASA.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji,
Mhandisi Anthony Sanga (katikati kulia) akimkabidhi nyaraka za
makabidhiano ya Ofisi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi
Leonard Msenyele (kushoto). Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi MWAUWASA, Christopher Gachuma (wa pili kushoto) na Makamu
wake, Edith Mudogo (wa kwanza kulia).

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji,
Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) mara baada ya kumkabidhi Ofisi Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele. Awali
Mhandisi Sanga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA na Mhandisi
Msenyele alikuwa Meneja Miradi MWAUWASA.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (aliyekaa) akiwa katika picha ya
pamoja na Mwenyekiti wa Bodi, Christopher Gachuma (nyuma katikati) na
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi MWAUWASA mara baada ya kukabidhiwa rasmi
Ofisi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji,
Mhandisi Anthony Sanga akizungumza na wafanyakazi wa MWAUWASA (hawapo
pichani) mara baada ya kukabidhi Ofisi. Wengine katika picha ni
Mwenyekiti wa Bodi, Christopher Gachuma (katikati) na Wajumbe wa Bodi ya
MWAUWASA.

Baadhi ya wafanyakazi wa MWAUWASA
wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga
(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukabidhi
Ofisi. Awali Mhandisi Sanga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji MWAUWASA.
0 comments:
Post a Comment