
Na. Paschal Dotto-MAELEZO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amezitaka nchi wanachama
wa Shirika la Mashirikiano ya kisheria kwa nchi za Asia na Afrika
(AALCO) kuimarisha ushirikiano na mshikamano katika kuendeleza sheria za
kimataifa kwa manufaa ya nchi hizo.
Akizungumza katika Mkutano wa
58 wa Mwaka wa AALCO, uliofanyika Jijijni Dar es Salaam Makamu wa Rais
amesema kuwa ni vizuri kwa taasisi hiyo ambayo inafanya kazi katika nchi
za Asia na Afrika kuimarisha mshikamano ili kukuza sheria za kimataifa
ambazo zitaleta Amani duniani.
“Napenda kuwaasa Nchi
wanachama wa Shirika hili kuwa mnatakiwa kuendeleza Ushirikiano,
Mshikamano na ushirikishwaji wa nchi zote katika masuala ya kisheria
ili kukuza na kuendeleza sheria za kimataifa kupitia Taasisi ya AALCO”,
alisema Makamu wa Rais.
Aidha Makamu wa Rais alisema
kuwa AALCO ina umuhimu mkubwa kwa nchi za Asia na Afrika kwani inaleta
mapinduzi makubwa na kuendeleza sheria za kimataifa ambazo zinasaidia
katika masuala mbalimbali ya kikanda.
Aliyataja masuala hayo ni kama
na kuimarisha Sheria za Biashara hususani kwenye biashara za kimataifa,
kuleta umiliki wa mali kwa nchi husika na kulinda usalama wa kikanda
katika nchi wanachama wa AALCO.
Mhe. Samia alisema kwamba
mwaka 1956 ilikuwa na jukumu kubwa la kuendeleza ukuaji wa Sheria za
kimataifa kwa bara za Asia na Afrika ambayo ilileta faida kubwa ya
ukomavu wa Sheria katika ukanda huo.
“Mkutano huu ambao ni mara ya
Kwanza kufanyika Tanzania unaonyesha jinsi gani Tanzania ilishiriki
katika kukuza Sheria za kimataifa kwa Kushirikina na AALCO ambapo
kupitia Shirika hilo Tanzania iliweza kusaidia kupatikana kwa uhuru kwa
nchi za kusini mwa Afrika.
Pia alisemanchi yetu imekuwa
nchi yenye Amani na majirani zake, imekuwa nchi ambayo inadumisha na
kujenga Amani kwenye nchi mbalimbali, kwa hivyo ni dhahiri kuwa Tanzania
inafanya kazi kwa karibu na AALCO kuendelea kufaidi matunda yake.
Kwa Niaba ya watanzania wote
Mhe. Samia aliwakaribisha wageni waliofika katika mkutano kwani ni
ishara ya kuendelea kumuunga mkono katibu Mtendaji wa AALCO Prof.Kennedy
Gastorn tangu Aingie katika utendaji huo mwaka 2016.
Aidha, Mhe. Samia alisema kuwa
uzoefu wa Tanzania katika mikutano mbalimbali ya kisheria na
ushuluhishi ikiwemo Mkutano wa Bandung na NAM umeiwezesha Tanzania kuwa
msuluhishi na mjenzi mkuu wa Amani katika nchi mbalimbali, lakini pia
Tanzania imekuwa ni nyumbani kwa wakimbizi wengi ambao nchi zao zina
machafuko.
Alieleza kuwa katika hatua
kubwa ya ushirikiano kati ya Tanzania na AALCO Tanzania imekuwa mstari
wa mbele katika kupambana na rushwa, baishara haramu ya kusafirisha
bidamu na utakatishaji fedha kwa nchi wanachama wa AALCO.
Makamu wa Rais aliwahakikishia
wageni wa mkutano huo kuwa Tanzania ni nchi salama na yenye watu wenye
ukarimu wa hali ya juu hivyo akawataka wasisite kuja kuitembelea kwani
ina vivutio mbalimbali ambavyo havipatikani sehemu nyingine nyoyote
duniani.
Pia aliwahakikishia wajumbe
kuwa nchi hii ni kituo kikubwa na kivutio kikubwa cha uwekezaji katika
Nyanja mbalimbali za maendeleo, hivyo akawakaribisha kuja kuwekeza
pamoja na kuja kufanya biashara.
0 comments:
Post a Comment