![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/40138223-5674-414a-b9cc-85cafbeaad49-1.jpg)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akishuhudia wakati mkewe Mary alipojiandikisha kwa ajili ya uchaguzi
ujao wa Serikali za Mitaa kwenye kituo cha Shule ya Msingi ya Nandagala
wilayani Ruangwa, Oktoba 12, 2019. Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama
Mary Majaliwa na kulia ni Mwandikishaji wa kituo hicho, Shaka Msange.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/c88e24d7-76bd-413d-9de1-9b5ffd20bf00-1.jpg)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa akizungumza na Binti Mkumba baada ya kujiandikisha kwa ajili
ya Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa kwenye kituo cha Shule ya Msingi
ya Nandagala wilayani Ruangwa, Oktoba 12, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/1c9603a9-cfa6-4394-87c6-d68a62ff035d-1.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/1c9603a9-cfa6-4394-87c6-d68a62ff035d-1.jpg)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akishuhudia wakati mkewe Mary alipojiandikisha kwa ajili ya uchaguzi
ujao wa Serikali za Mitaa kwenye kituo cha Shule ya Msingi ya Nandagala
wilayani Ruangwa, Oktoba 12, 2019. Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama
Mary Majaliwa na kulia ni Mwandikishaji wa kituo hicho, Shaka Msange.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
*************************************
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amejiandikisha kwenye kituo cha shule ya msingi
Nandagala, wilayani Ruangwa, Lindi ili aweze kushiriki uchaguzi wa
Serikali za Mitaa.
Waziri Mkuu
ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa amejiandikisha kijijini kwao leo
asubuhi (Jumamosi, Oktoba 12, 2019) akiwa na mkewe Mama Mary Majaliwa.
Akizungumza
na wakazi wa kijiji hicho, Waziri Mkuu amesema zoezi la kujiandikisha ni
la kitaifa na ni haki ya kila Mtanzania ili aweze kuchagua kiongozi
amtakaye au aweze kugombea kwenye uchaguzi utakaofanyika Novemba 24,
mwaka huu.
“Kila mmoja
anapaswa kuja kujiandikisha. Zoezi hili ni tofauti na lile la uchaguzi
mkuu. Kuna watu wanafanya upotoshaji wa makusudi, wanawadanganya wenzetu
kwamba kama una kadi ya uchaguzi huna haja ya kujiandikisha. Hii siyo
kweli, hiyo kadi ni ya uchaguzi wa mwakani,” amesema.
“Nawasihi mje
kujiandikisha ili muweze kuchagua viongozi mnaowataka. Zoezi hili
limebakiza siku mbili tu, mwisho wake ni tarehe 14 Oktoba, 2019 jioni.”
Amesema mtu
yeyote aliyefikisha miaka 18, ana haki ya kujiandikisha ili aweze kuwa
mgombea au mpiga kura, na pia awe na uhakika kuwa amemchagua kiongozi
anayemtaka.
Mara baada ya
kujiandikisha, Waziri Mkuu alipita katika vijiji vya Chimbila B,
Chimbila A, Michenga (Jerusalem), Michenga (Misri), Nangumbu na
Nanganga.
Akiwa njiani,
alizumgumza na wanavijiji waliosimama njiani walipoona msafara wake na
akatumia fursa hiyo kuwahimiza wajiandikishe kwa ajili ya uchaguzi ujao
wa Serikali za Mitaa.
“Wana-Ruangwa
tutumie fursa hii ili tuchague viongozi watakaokereketwa na kuleta
maendeleo. Tuchague viongozi ambao hata wakipewa fedha za miradi,
watazitumia kwa maendeleo na hawatashawishika kirahisi kuzitumia kwa
maslahi yao binafsi.”
“Kuna fedha
zinaletwa hapa shilingi milioni 60 za elimu, tunaleta fedha za kuchimba
visima lazima wazisimamie, tunaleta fedha za afya, lazima wazisimamie.
Tunahitaji watu ambao watakuwa waaminifu na wanaoweza kusimamia miradi
yetu.”
“Tunatakiwa
tuchague viongozi watakaosimamia maendeleo, wanaohamasisha maendeleo.
Tunatakiwa tuchague viongozi ambao ni waadilifu, waaminifu, wachapakazi,
wasikivu, wapenda watu na wanaoweza kusimamia fedha zinazoletwa hapa.
Ninyi mnawafahamu kwa sababu mnaishi nao,” amesema.
Katika maeneo
yote hayo, Waziri Mkuu aliwaeleza kwamba Serikali imetoa fedha za
kununua taa za barabarani ambazo zimeanza kusambazwa na zikishafungwa,
zitawawezesha wajasiriamali wafanye biashara zao hadi usiku.
“Tunaboresha
vijiji vyetu kuanzia Nanganga, Nangumbu, Michenga (Misri), Michenga
(Jerusalem), Chimbila A na B, Chikunji, Mtope, Likunja, Nkowe,
Nandagala, Namichiga na Mandawa.
0 comments:
Post a Comment