Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akifafanua
jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara Mkoani Iringa kwa lengo la kukagua
miradi ya vijana iliyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. (Wa tatu
kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na
Sheria Mhe. Najma Giga (Mb).
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya
Katiba na Sheria wakisikiliza taarifa ya Mkurugenzi wa Kiwanda cha
EatFresh Bi. Hadija Jabiry (hayupo pichani), walipofanya ziara Mkoani
Iringa kwa lengo la kutembelea miradi ya Vijana iliyonufaika na Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Kusindika Mbogamboga na Malimbichi cha EatFresh Bi. Hadija Jabiry
(kulia) akiwaeleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba
na Sheria wakati walipotembelea kiwanda hicho kilichopo eneo la SIDO,
Mkoani Iringa.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha EatFresh wakiendelea na kazi ya kuchambua maharage mabichi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga (Mb) akieleza jambo wakati
Kamati hiyo ilipokutana na watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Iringa kwa ajili ya kupokea taarifa kuhusu miradi ya vijana iliyonufaika
na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Katiba na Sheria wakisikiliza taarifa ya vikundi vya vijana
vilivyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kutoka kwa Mkuu wa Wilaya
ya Iringa Mhe. Richard Kasesela (hayupo pichani), walipofanya ziara
Mkoani Iringa kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Mfuko huo.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Katiba na Sheria wakisikiliza taarifa ya vikundi vya vijana
vilivyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kutoka kwa Mkuu wa Wilaya
ya Iringa Mhe. Richard Kasesela (hayupo pichani), walipofanya ziara
Mkoani Iringa kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Mfuko huo na
kutembelea miradi ya vikundi vya vijana. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi
ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya
Katiba na Sheria Mhe. Ally Saleh (kulia) akichangia jambo kuhusu miradi
itakayowanufaisha watu wenye ulemavu kunufaiaka na Mfuko huo wa
Maendeleo ya Vijana.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.
Richard Kasesela (wa pili kutoka kulia) akieleza jambo kwa Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipofanya ziara ya
kutembelea miradi ya vijana iliyonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya
Vijana, Mkoani Iringa. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde. Kulia ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga (Mb).
Kiongozi wa Kiwanda cha vijana cha
EnviBright Bw. Paul Myovela (kulia) akitoa maelezo kwa Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria namna wanavyotengeneza
mbolea inayotokana na taka ngumu.
Muonekano wa Kiwanda cha EnviBright kinachojihusisha na utengenezaji wa mbolea kupitia taka ngumu.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
0 comments:
Post a Comment