Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akihutubia wanachi waliyohudhuria katika Uzinduzi wa Mafunzo kwa vijana
kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba uliofanyika katika Viwanja vya
Nanenane, Mkoani Lindi Oktoba 10, 2019.
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Lindi
wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majiliwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mafunzo kwa vijana kwa kutumia
teknolojia ya Kitalu Nyumba yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane,
Mkoani Lindi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Uzinduzi
wa Mafunzo kwa vijana kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba
yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane, Mkoani Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe.
Godfrey Zambi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mafunzo kwa vijana kwa
kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba yaliyofanyika mkoani humo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizindua jiwe la Msingi kuashiria kuzinduliwa rasmi Mafunzo kwa vijana
kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba.
Muonekano wa Kitalu nyumba kilichozinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majiwa katika Viwanja vya Nanenane, Ngongo Mkoani Lindi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiangalia Kitabu cha Historia ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage
Nyerere alipotembelea banda la Maonesho la Taasisi ya Kumbukumbu ya
Mwilimu Nyerere mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Mpilipili.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza jambo na kikundi cha International Youth Fellowship
alipotembelea Banda la Maonesho la kikundi hicho wakati wa maadhimisho
ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayoendelea Mkoani Lindi. Kulia ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
Baadhi ya Vijana wa Skauti wakipitia na jumbe mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika Mkoani Lindi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikata utepe kuashiria kufungua maadhimisho ya 17 ya Wiki ya Vijana
yanayofanyika Mkoani Lindi katika viwanja vya Mpilipili. (Wa pili kutoka
kulia) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, na Mwakilishi wa
UNFPA Bi. Tausi Hassani. (Wa nne kutoka Kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi,
Mhe. Godfrey Zambi na Waziri wa Vijana, Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Balozi Ali Karume.
Msanii wa Mziki wa Kizazi kipya
Kala Jeremiah ambaye pia ni Balozi wa Vijana akiimba pamoja na vijana
wakati wa maadhimisho ya wiki ya vijana.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa
kwenye picha ya pamoja na wadau wa Asasi za Vijana mara baada ya
kuzindua wiki ya vijana Mkoani Lindi Oktoba 10, 2019.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
…………………..
Na; Mwandishi Wetu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
amezitaka halmashauri kuwawezesha vijana mikopo ya asilimia 4% ya mapato
ya ndani wanayotenga kwa ajili ya kuwawezesha vijana kujenga Vitalu
Nyumba (Green House) vyao binafsi.
Ametoa kauli hiyo leo Oktoba 10,
2019 wakati wa Uzinduzi wa Mafunzo kwa Vijana ya Kilimo cha Kisasa kwa
kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba katika Viwanja vya Nanenane, Ngongo
Mkoani Lindi.
Waziri Mkuu amesema vijana ni
rasilimali muhimu katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo katika jamii,
hivyo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli aliamua kuwajengea vijana mazingira wezeshi ikiwemo
kupata fursa za mikopo na ujuzi unahitajika ili waweze kushiriki
kikamilifu katika shunguli za kimaendeleo.
Alieleza kuwa, Serikali iliamua
kuanzisha utaratibu wa kila halmashauri kutenga asilimia 10% ya mapato
yake kwa lengo la kutoa mikopo isiyo na riba kwa vijana asilimia 4%,
wanawake asilimia 4% na wenye ulemavu asilimia 2%.
“Halmashauri zote zihakikishe
zinatenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kuwawezesha vijana ili waweze
kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo shughuli za kilimo zitakazowasaidia
kujiajiri na kujiingizia kipato,”
Alifafanua kuwa sekta ya kilimo
ndiyo kimbilio la wananchi wengi na kwa kutumia teknolojia ya kitalu
nyumba vijana wengi watapata ajira katika sekta hiyo kwa kuwa ina faida
kubwa sana ikiwemo kupata mazao mengi katika eneo dogo na kupata mazao
bora yanayokidhi viwango katika soko la ndani nan je ya nchi.
Waziri Mkuu aliongeza kuwa
Serikali kupitia Ofisi yake imeendelea kuratibu programu ya ukuzaji
ujuzi nchini na imeanza kutoa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa kutumia
teknolojia ya Kitalu Nyumba katika Mikoa yote na Halmashauri zote
nchini.
Aidha alitoa wito kwa vijana
kuendelea kujitokeza kwa wingi katika kuchangamkia fursa za mafunzo ya
stadi mbalimbali za kazi kupata ujuzi stahiki utakaowawezesha kushindana
katika soko la ajira.
“Nimefarijika kuona vijana
waliopata mafunzo haya katika awamu ya kwanza wamekuwa na uwezo wa
kujenga vitalu nyumba kwa ajili ya watu wengine waliotambua umuhimu wa
kilimo cha aina hiyo, fursa hiyo ni ishara tosha kuwa vijana wameimarika
katika mafunzo hayo,”
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu
alizindua Maadhimisho ya 17 ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyofanyika
katika Viwanja vya Mpilipili na amewasihi vijana kuwa wazalendo na
kutambua mchango wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika
kuleta maendeleo ya nchi yetu na bara la afrika kwa ujumla.
Kwa Upande wake Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alieleza kuwa
Serikali imetoa kutoa mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa kwa teknolojia
ya kitalu nyumba katika halmshauri zote nchini ambapo katika awamu ya
kwanza mradi huo umefika katika halmashauri 83 hadi sasa lengo ni
kufikisha ujuzi huo kwa vijana zaidi ya 18,000.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe.
Gogfrey Zambi alisema kuwa vijana katika mkoa huo wamehamasika na mradi
huo kwa kuwa wametambua una manufaa kwao.
“Programu hii imekuja wakati
sahihi na imesaidia vijana kwa kiasi kikubwa kwa kuzingatia mafanikio
yatokanayo na kilimo hiki cha kisasa kinacholeta tija,” alisema Zambi
Pamoja na hayo, Mkuu wa Mkoa
alielezea hali ya usalama katika mkoa huo kulekea kwenye Maadhimisho ya
Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zinazotarajiwa kufanyika Mkoani humo.
Pia Kijana Mmoja wapo aliyenufaika
na mafunzo hayo Bw. Azizi Njenje ameishukuru Serikali kwa kuwapatia
mafunzo hayo ambayo yamewajengea uwezo wa kujiamini na kuwafanya kuwa
chachu katika kushiriki kwenye shughuli za kilimo.
0 comments:
Post a Comment