Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na
Ugani kutoka wizara ya mifugo Dkt.Angello Mwillawa,akifafanua jambo kwa
washiriki sehemu ya pili ya mafunzo rejea kwa wataalam wa malisho kutoka
mashmba ya serikali na wadau wa malisho nchini wakati akifundishi mada
mbalimbali zinazohusiana na malisho kushoto kwake ni Afisa mifugo Mkuu
Idara ya malisho na Rasilimali ya vyakula vya mifugo Israel Kilonzo
yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na
Ugani kutoka wizara ya mifugo Dkt.Angello Mwillawa,akifundisha mada
mbalimbali kwa washiriki sehemu ya pili ya mafunzo rejea kwa wataalam wa
malisho kutoka mashmba ya serikali na wadau wa malisho nchini
yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na
Ugani kutoka wizara ya Mifugo Dkt.Angello Mwillawa,akiwaonyesha
washiriki wa semina ya mafunzo rejea kwa wataalam wa malisho kutoka
mashamba ya serikali na wadau wa malisho nchini walipotembelea shamba la
malisho TALIRI lililopo Vianze yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika
chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
………………….
Na Alex Sonna, Mpwapwa
MAFUNZO rejea kwa wadau na
wataalam wa malisho kutoka mashamba ya serikali nchini, yamehitimishwa
,huku Wizara ya Mifugo ikisisitiza uzalishaji wa mashamba ya malisho
bora.
Mafunzo haya ya siku mbili yamefanyika katika Chuo cha LITA kampasi ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Akizungumza leo baada ya
kuhitimisha mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani kutoka
Wizara hiyo, Dk.Angello Mwillawa, amesema lengo la uzalishaji huo ni
kuwa na malisho yanayozaa kwa wingi na yana ubora unaomsaidia mnyama
kupata virutubisho sahihi.
“Wizara imeona umuhimu wa jambo
hili kwa kushirikiana na taasisi zake imewaleta pamoja watendaji na
wataalam katika mafunzo hayo ili kuwa na mikakati ya kuzalisha malisho
bora,”amesema.
Aidha, amesema kumekuwepo na
mikakati mbalimbali ya wizara ikiwa ni pamoja na udhibiti wa magonjwa ya
mifugo na matumizi ya madawa na viuatilifu kuhakikisha mifugo ipo
katika ubora unaotakiwa.
Amesema Wizara imekuwa ikitekeleza
mkakati wa upatikanaji wa malisho na maji kwa nchi nzima, jambo ambalo
limekuwa likitiliwa mkazo na Wizara hiyo namna bora ya kuhakikisha
nyanda za malisho na maeneo ya machunga yanaboreshwa ili kujitosheleza
na malisho mwaka mzima.
“Tumekuwa tukihakikisha zile
nyanda zetu za malisho wafugaji wanapata elimu ya kutosha na watumiaji
wengine wa nyanda za malisho kwa kuhakikisha kunakuwa na matunzo na
matumizi endelevu ya malisho,”amesema.
Naye, Afisa Mifugo Mkuu Idara ya
malisho na rasilimali ya vyakula vya mifugo kutoka wizara hiyo, Israel
Kilonzo, ameongeza kusema kuwa mafunzo hayo ni kuwa na uelewa wa pamoja
katika uzalishaji wa malisho na kutunza nyanda za malisho.
“Wazingatie yale waliyofundishwa
waende kufanya kazi ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea katika
kuhakikisha tunazalisha malisho ya kutosha,”amesema.
Kwa upande wake, Mkuu wa kampas ya
LITA Mpwapwa, Moses Mlahagwa, amesema ili mifugo izalishe maziwa na
nyama ya kutosha lazima wapate chakula cha kutosha.
“Hii imekuwa ni changamoto katika
uzalishaji mazao ya mifugo yamekuwa ni hafifu kwasababu hakuna lishe ya
kutosha, hapa kwenye mafunzo tumeona changamoto hizi sasa tunaweza
kuchukulia kama fursa ya kupiga hatua kwenye uzalishaji,”amesema
Hata hivyo, amesema chuo hicho
kipo kwenye mpango kuwa na maeneo makubwa ya uzalishaji malisho hivyo ni
fursa nzuri kwao kuhakikisha wanaingia kwenye eneo la uzalishaji kwa
kupata uzoefu wa kutosha kutoka kwa wadau wengine.
Kadhalika, Meneja masoko kutoka
Ranchi za Taifa(Narco), Mzava Emmanuel, amesema kuna wakati nchi iliwahi
kukumbwa na ukame na mifugo kufa haipaswi kujirudia tena kwa kuwa
wataalam wapo.
“Tufike sehemu kama taifa tuwe na
ghala la malisho hata itakapotokea njaa ya malisho kwa miaka miwili
kusiwe na mifugo inayokufa bali walishwe kupitia hifadhi ya malisho
itakayokuwepo,”amesema.
Nao baadhi ya washiriki,
Wameshukuru Wizara kwa kuwapatia mafunzo hayo yatakayosaidia kupiga
hatua katika kuhakikisha kunakuwepo na malisho ya kutosha kwa ajili ya
mifugo.
Afisa Mifugo kutoka shamba la
mifugo Mabuki na mtaalam wa malisho, Asteria Mwaya amesema ili kuwa na
mbegu bora ya malisho kunapaswa shamba liandaliwe vyema, kuvunwa na
kuhifadhiwa vizuri.
“Tumepata ujuzi ambao unatusaidia
kufanya kazi eneo lolote hata kama una rasilimali chache unaweza kufanya
vizuri na kwa tija, na kusaidia kutoa elimu kwa wananchi kuondokana na
uingizaji ng’ombe kwenye shamba la serikali na kujitengenezea malisho
yao wenyewe,”amesema.
0 comments:
Post a Comment