Mkazi
wa Mbezi Africana Dar es Salaam, Amani Elikana (32), amefikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akituhumiwa kumuua Askari wa
Usalama Barabarani, Sajenti Mensali wa Kituo cha Polisi Mabatini –
Kijitonyama.
Akisoma
hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu, Caroline Kiliwa, Wakili wa
Serikali, Amani Mghamba alidai mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Julai
22 mwaka huu eneo la Kijitonyama.
“Mtuhumiwa
inadaiwa kwamba siku hiyo kwa makusudi ulimuua askari mwenye namba D.
8254 Sajenti Mensali kinyume cha sheria ya Jamhuri ya Muungano,” alidai Mghamba.
Hakimu
Kiliwa alisema mtuhumiwa hapaswi kujibu kitu chochote kwa kuwa mahakama
hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hivyo shtaka hilo
liliahirishwa hadi Oktoba 4 mwaka huu litakapotajwa tena.
0 comments:
Post a Comment