Vodacom
Tanzania wakishirikiana na Benki ya CBA, ilizindua promosheni kubwa
inayojulikana kama "Jiongeze na M-Pawa" ambayo inawawezesha watumiaji wa
huduma ya M-Pawa kujishindia zawadi ya fedha taslimu.
Jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya promosheni hiyo na mshindi mmoja wa droo kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100.
Jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya promosheni hiyo na mshindi mmoja wa droo kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100.
Washindi wa wiki watazawadiwa shilingi milioni 20 na washindi wa siku watazawadiwa shilingi milioni moja.
Promosheni
hiyo ambayo ilianza mwanzoni mwa mwezi wa 9 itadumu kwa kipindi cha
wiki sita na itafikia kilele mwishoni mwa Mwezi Oktoba, 2016.
Meneja
masoko Huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania ,Noel Mazoya (katikati)
akiongea na mmoja wa mshindi wa droo ya promosheni ya Jiongeza na
M-Pawa wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika
jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha Isaack Pilemon alijishindia
kitita cha shilingi Milioni 20. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni
Meneja wa Huduma za M-Pawa wa Benki ya CBA Eric Luyangi na Msimamizi
wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari Maggid.
Meneja
masoko Huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania ,Noel Mazoya (katikati)
akiwaonyesha waandishi wa habari namba ya mshindi wa droo ya
promosheni ya Jiongeza na M-Pawa wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya
pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha
Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20.
Wanaoshuhudia
kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma za M-pawa wa Benki ya CBA Eric
Luyangi na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari
Maggid. Hadi sasa washindi 2,800 wameongezea mara mbili ya akiba zao
za M-Pawa washindi 14 wameshinda milioni 1 kila mmoja na washindi 2
wamejishindia milioni 20 mshindi wa jumla washilingi milioni 100
atapatikana mwezi wa kumi.
Waandishi
wa habari wakifuatilia tukio la kuchezesha wa droo ya promosheni ya
Jiongeza na M-Pawa wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki
iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo ambapo mkazi wa Arusha Isaack
Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20.
0 comments:
Post a Comment