Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Zainab Chaula akizungumza na
viongozi wa Wizara yake pamoja na viongozi kutoka Shirika la Maendeleo
GIZ LA Nchini Ujerumani katika hafla ya kutiliana saini makubaliano ya
Uboreshaji sekta ya afya.
Mwakilishi wa Serikali ya
Ujerumani.Bi. Vera Rosendahl akiongea wakati wa kusaini mkataba kati ya
nchi yake na Serikali ya Tanzania
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
GIZDkt. Mike Falke akisaini mkataba wa makubaliano na serikali ya
tanzania kupitia wizara ya afya katika kuimarisha afya ya msingi nchini,
kushoto ni katibu mkuu wa wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Zainab Chaula akibadilishana mkataba na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Maendeleo GIZ, Dk Mike Falken
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Zainab Chaula akiwa na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Maendeleo GIZ, Dk Mike Falken katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshika hati za mikataba
…………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesaini mkataba wa makubaliano wa miaka
mitatu na serikali ya Ujerumani kwa ajili ya kuimarisha afya ya msingi
nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Dkt. Zainabu Chaula alisema kuwa wizara yake imesaini mkataba huo na
serikali ya Ujerumani katika kuboresha sekta ya afya katika maeneo manne
ambapo sekta hiyo itapata kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni
26.6.
” Kwa kweli niwashukuru sana wenzetu
wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani kwa namna ambavyo wamekua bega
kwa bega na sisi, zaidi niwapongeze na kuwashukuru ndugu zetu wa GIZ
hawa wamekua wadau wakubwa wa Afya nchini.
” Tunawaahidi kuwapa ushirikiano na
kusimamia kwa ukamilifu yale yote tuliyokubaliana kuyatekeleza, lengo
letu sote ni kuona sekta hii ya afya inakua na inawanufaisha Watanzania
ambao ndio haswa walioipa dhamana Serikali ya awamu ya tano
kuwatumikia,” Amesema Dk Chaula.
Aidha amelipongeza Shirika hilo kwa
kukubali kuwapatia fedha hizo kwa wakati mmoja ili iwe rahisi kuweza
kutekeleza maazimio yote kwa haraka na kwa ufanisi zaidi.
” Ndugu zangu kazi ya Serikali ni
kuwaletea wananchi wake Maendeleo na Rais wetu Dk John Magufuli ni mtu
wa vitendo haswa, amedhamiria kuifanya Nchi yetu kuwa imara katika kila
nyanja na afya ikiwemo, haya yote tunayoyafanya leo ni matokeo ya juhudi
kubwa ambazo yeye kama Kiongozi wetu wa Nchi amekua nazo,” Amesema Dk
Chaula.
Naye Mkurugenzi mkazi wa Shirika la
Maendeleo GIZ, Dk Mike Falken amesema makubaliano waliyoyafikia na
Wizara ya Afya ni matokeo ya utendaji kazi wa Serikali ya Tanzania
katika kuwatumikia wananchi wake.
Aidha Dk.Falken amesema kuwa mkataba
huo umejikita katika afya ya msingi hasa katika zahanati na vituo vya
afya na utalenga maeneo matano ambayo ni Uboreshaji wa Taarifa, Mama na
Mtoto, Bima, Uzazi wa Mpango na Utawala Bora.
” Sisi tunawaahidi kuendeleza
ushirikiano uliopo kati yetu, sisi tunaridhishwa na kasi ya Rais
Magufuli katika kuwatumikia Watanzania na ni wazi tunamuunga mkono kwa
vitendo,” amesema Dk Falken.
Awali Shirika hilo lilikabidhi kwa Serikali kupitia Wizara ya Maji mradi wa Maji katika eneo la Nghong’onha jijini Dodoma ambao umegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 331 na utahudumia wananchi takribani 12000.
0 comments:
Post a Comment