Chama cha
mapinduzi Mkoani Geita kimelitaka jeshi la zima moto na uokoaji Kuomba
radhi ndani ya siku saba kutokana na tuhuma ambazo zilielekezwa kwa
viongozi wa chama hicho kuingilia kazi na utendaji wa jeshi hilo.
Hayo
yamesemwa na Mjumbe wa halmashauri kuu
ya Taifa(NEC) Iddi Kassim Iddi,wakati alipokuwa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya mkoa ya chama
hicho,alisema wao kama chama wamepokea kwa masikitiko makubwa tuhuma hizo
ambazo zimeelekezwa kwenye chama hicho na
lengo lilikuwa sio kuingilia majukumu ya jeshi hilo ila ni kuwatetea
wananchi wa Rwamgasa ambao walikuwa
wakiuziwa mitungi kwa bei kubwa
bila ya kupatiwa risti ya serikali.
“Watambue ya
kuwa sisi chama na serikali ni kama baba na mwana ni kwamba ni lazima kuhakikisha kwamba
tunafanya kazi kwa pamoja na napenda kukanisha kuwa sisi hatuna uadui wala na
jeshi la zima moto na tunampa siku saba akiombe radhi chama na viongozi wake
kwani namna ambavyo amefanya ni kuchafuana”Alisema Kassim.
Aidha Katibu mwenezi wa chama hicho Mkoani humo,Devid Azaria ,amekanusha juu ya
tuhuma za viongozi wa chama kuingilia
zoezi lao na kwamba wanachokikataza ni taratibu ambazo zilitumika za uuzwaji wa
vifaa vya kuzimia moto kuwa zilikuwa za kuwalazimisha wachimbaji bila ya kuwapa
elimu jambo ambalo sio sahihi.
Hata hivyo
mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Humo.Alhaji Saidi Karidushi amewataka viongozi
wote kufanya kazi kwa kutimiza majukumu yao na kwamba kama kuna tatizo ni vyema
wakayashughulikia wao bila ya kutegemea nguvu kutoka kwake.
Kwa upande
wake Kamanda wa Jeshi la Zima Moto na uokoaji mkoani Geita Bw Elisa Mugisha alipopigiwa
simu na mtandao huu amekiomba radhi chama cha Mapinduzi huku akisisitiza kuwa
baadhi ya viongozi wanaomiliki makarasha kulipia tozo zinazotakiwa na jeshi la
zima moto ili kuepusha mtafaruku baina ya pande hizo mbili.
0 comments:
Post a Comment