Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Momba wakati
akikagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Mazao la Kakozi lililopo Wilaya
ya humo.
Mafundi wakiendelea kuchimba
msingi katika ujenzi wa Soko la Mazao la Kakozi lililopo Wilayani ambapo
ujenzi wa Soko hilo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja na
kugharimu shillingi bilioni nane.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela akikagua mchoro wa Soko la Mazao la Kakozi lililopo
Wilaya ya Momba ambapo kukamilika kwa ujenzi wa Soko hilo kutasiadia
wakulima kuuza mazao yao kwa bei nzuri.
Mafundi wakiendelea kuchimba
msingi katika ujenzi wa Soko la Mazao la Kakozi lililopo Wilayani ambapo
ujenzi wa Soko hilo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja na
kugharimu shillingi bilioni nane.
……………………
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela ameagiza ujenzi wa Soko la Mazao la Kakozi lililopo
Wilaya ya Momba ufanyike mchana na usiku kutokana na kuchelewa kuanza.
Brig. Jen. Mwangela ametoa agizo
hilo jana jioni alipotembelea eneo la ujenzi wa Mradi huo na kukagua
maendeleo ya ujenzi huo ambao mpaka kukamilika kwake utagharimu shilingi
shilingi bilioni 8 na mpaka sasa serikali imetoa shilingi bilioni 2.
“Naagiza ujenzi huu ufanyike
Mchana na Usiku kwani tuko nyuma ya muda kwa Zaidi ya miezi mitatu,
Mkurugenzi hakikisha hilo linafanyika na Tanesco ninawaelekeza waweke
umeme hapa ili mafundi hawa wakamilishe kazi hii kwa muda muafaka”,
ameelekeza Brig. Jen. Mwangela.
Ameongeza kuwa ujenzi wa Soko hilo
la mazao ni Mkombozi kwa wakulima wa Wilaya ya Momba na Mkoani Songwe
kwani watapata sehemu ya kukusanyia mazao ya na kuyauza kwa bei sahihi
kuliko kufuatwa na walanguzi mashambani ambao huwapunja.
“ Soko hili litawaokoa wakulima
hawana mahali pa kuuzia mazao yao, kuna wao wanaenda huko wanawadanganya
na kuchukua mazao yao kwa bei nafuu sana lakini Mkulima wetu akipata
nafasi ya kufikisha mazao yake katika soko hili akaja kuyauza mwenyewe
atauza kwa bei nzuri”, amesisitiza Brig. Jen. Mwangela
Aidha amewataka mafundi
wanaojenga soko hilo kuonyesha ufundi wao kwa kujenga kwa viwango na kwa
kasi nzuri ili wakulima wanufaike na mafundi nao wanufaike kwa
kukamilisha ujenzi kwa muda mfupi ili wapate faida.
0 comments:
Post a Comment