Mkuu wa Idara ya Utafiti Mkakati
na Machapisho kutoka ESRF, Profesa Fortunata Makene, akiwasilisha mada
wakati wa warsha hiyo ya kujadili namna ya kutatua changamoto za watoto
na vijana katika majiji na miji, warsha iliyofanyika jijini Dodoma
tarehe 11 Septemba 2019.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto
kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mwajuma
Magwiza, akiongea wakati akifungua warsha hiyo ya kujadili namna ya
kutatua changamoto za watoto na vijana katika majiji na miji, warsha
iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 11 Septemba 2019.
Mkuu wa Sera za Hifadhi za Kijamii
kutoka UNICEF, Dkt, Paul Quarles Van Ufford, akiwasilisha maada wakati
wa warsha hiyo ya kujadili namna ya kutatua changamoto za watoto na
vijana katika majiji na miji, warsha iliyofanyika jijini Dodoma tarehe
11 Septemba 2019.
Mtaalam wa Ufatiliaji na Tathmini
kutoka UNICEF, Vu Manh Hong, akiwasilisha mada wakati wa warsha hiyo ya
kujadili namna ya kutatua changamoto za watoto na vijana katika majiji
na miji, warsha iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 11 Septemba 2019.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria
warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa warsha
hiyo ya kujadili namna ya kutatua changamoto za watoto mtoto na vijana
katika majiji na miji, warsha iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 11
Septemba 2019.
Meza kuu wakifuatilia mawasilisho
mada wakati wa warsha hiyo ya kujadili namna ya kutatua changamoto za
watoto katika majiji na miji, warsha iliyofanyika jijini Dodoma tarehe
11 Septemba 2019.
Mchumi Mkuu, Wizara ya Fedha na
Mipango ambaye pia ni Mwenyekiti wa Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania
(TULab) Dkt. Lorah Madete, akiwasilisha mada wakati warsha hiyo ya
kujadili namna ya kutatua changamoto za watoto na vijana katika majiji
na miji, warsha iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 11 Septemba 2019.
……………………..
Na .Alex Sonna, Dodoma.
Katika kuhakikisha changamoto za
watoto na vijana maeneo ya Mijini zinapatiwa ufumbuzi, leo tarehe 11
Septemba 2019 Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa
kushirikiana na UNICEF, kupitia Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania
(TULab), wamewakutanisha wadau na wataalam kutoka serikalini kujadiliana
namna ya kumlinda mtoto hasa maeneo ya mijini.
Akizungumza wakati wa Warsha hiyo
Mkuu wa Idara ya Utafiti Mkakati na Machapisho kutoka ESRF, Profesa
Fortunata Makene, amesema lengo la kukutana kwa wadau hao ni kupata
maoni yatakayosaidia kuanzisha programu itakayosaidia kutatua changamoto
za watoto na vijana ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mtoto analindwa.
Kwa kuweka mazingira mazuri katika majiji na miji.
Amesema warsha kama hii
iliofanyika Dodoma itafanyika pia Mikoa ya Dar es saalam na Mbeya,
ambapo watakutana na wadau kutoka Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali
(NGO’s), Sekta Binafsi pamoja na watoto wenyewe.
Amesema washiriki wa warsha ya leo
ni wataalam zaidi ya 20 kutoka serikalini yaani TAMISEMI, Ofisi ya
Takwimu, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto, Ofisi
ya Waziri Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, Chuo
Kikuu cha Dodoma nk., wote hawa wakiwa ni wadau wa ukuaji wa miji.
Ilielezwa katika kupanga miji ni
lazima mipango hiyo iwe rafiki kwa watoto ili isiweze kuwaathiri,
amesema watoto wamekuwa wakiathiriwa sana na ukuaji wa miji na hata
wengine kujiingiza katika mambo ambayo yanawaathiri na kushindwa kufikia
malengo yao.
Miongoni mwa changamoto
zilizotajwa katika miji ambazo zimekuwa zikiwaathiri au kuathiri ukuaji
kwa watoto ni pamoja na ajira za watoto, hii imetajwa kuwa ni
changamoto ambayo imekuwa ikiathiri watoto kwa sababu watoto wengi
wamekuwa wakijiingiza katika kutafuta kipato kujikimu.
Upatikanaji wa maji hasa kwa
maeneo ambayo hayajapimwa imekuwa ni changamoto kwa sababu watoto ndio
huenda kutafuta maji na huko ndio hukutana na vitendo ambavyo huwaathiri
katika ukuaji wao kwa matukio ya ukatili.
Mitandao ya kijamii pia imetajwa
kama ndio chanzo cha watoto wa mijini kuathiriwa katika ukuaji wao
tofauti na watoto wa vijijini, pia wadau wameshauri kuendelea kutoa
elimu kwa watoto ili waepukane na athari hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Idara
ya Maendeleo ya Watoto kutoka wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto, Mwajuma Magwiza, amesema serikali imekuwa ikifanya
jitihada mbalimbali ikiwamo kuanzisha dawati la watoto.
Pia uanzishwaji wa huduma ya simu
kwa watoto kupitia namba 116, ambayo mpaka sasa imesaidia kusikilizwa
kwa mashauri 43 ya watoto yakijumuisha ubakaji, mimba na ndoa za
utotoni, Pia wamefanikiwa kutoa huduma muhimu kwa watoto 329 wanaoishi
kwenye vituo vya
kulelea watoto.
Mgeni rasmi katika warsha hii
alikuwa Dr. John K. Jingu, Katibu Mkuu, Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto, ambaye aliwakilishwa na Mwajuma Magwiza,
Mkurugenzi, Maendeleo ya watoto.
0 comments:
Post a Comment