METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, September 25, 2019

RUMBESA YAWASONONESHA WAKULIMA WA VIAZI,VITUNGUU MBEYA


Na Bashiri Salum ,Mbeya
Wakulima wa  viazi na vitunguu katika kijiji cha Ntangano Ijombe kilichopo Mkoani Mbeya wameiomba Wizara ya Kilimo kuwasaidia kupata  mifuko maalumu itakayotumika kama Kipimo cha viazi ili kuepuka changamoto ya kujaza mifuko kupoita kiasi kunakofahamika kama  rumbesa
Wakiongea wakati wa mahojiano na Kitengo cha Mawasiliano mara baada ya kutembelewa shambani kwao hivi karibuni wamesema mifuko inayotumia kufungashia viazi na vituguu inakuwa na ujazo mkubwa kuanzia kilo 150 hadi 180  wakati wa kuwapimia wafanyabiashara .
 Aidha wamesema kwamba gharama za uzalishaji zimekuwa juu hivyo kwa kuuza viazi au vitunguu kwa rumbesa kunawatia hasara na kushindwa kurudisha gharama za uzalishaji.
Yohana Wilfredi Wangere moja ya mkulima   anayelima mahindi, ngano, viazi na vitunguu katika kijiji hicho   anasema amejenga nyumba kwa kupitia kilimo lakini isingekuwa changamoto hiyo ya masoko angekuwa amefanya mambo mengine makubwa zaidi.
 Bwana Yohana anaendelea kusema kwamba  wamepata changamoto ya ya kununua pembejeo kwa bei ya juu ambazo hutumika kwa wingi zaid mvua inapokuwa kubwa. 
Ameimba serikali kuongeza ruzuku katika pembejeo ili wakulima hao waweze kuzinunua kwa bei ndogo na kufanya kilimo chao kuwa na tija.
 wizara ya kilimo imeshauriwa kuwa na ushirikiano mkubwa na mamlaka ya hali ya hewa TMA ili kutoa taarifa mapema kwa wakulima kuhusu kiwango cha mvua kiatakachokuwepo katika mikoa ambapo wakulima wajipanga kununa pembejea kulngana na viwango vya mvua, alisema bwana Yohana.
Akiongea kwa niaaba ya Mrungezi wa kituo cha utafiti Uyole Bi Katheri Kabungo amesema kwamba kituo cha utafiti cha uyole TARI UYOE  kimekuwa kikitoa msaada mkubwa kwa wakulima wa maharage, viazi, ngano, pareto na mahindiili lengo likiwa ni kuongeza tija katika kilimo chao.
akiongea hali soko la wakulima wa mazao mbalimbali katika mikoa ya nyanda za juu anasema tatizo kubwa ni tija ndogo inayosababishwa na matumizi yasikuwa sahihi ya viuatilifu, kutotumia mbolea na mbegu bora za kilimo.
hata hivyo amesisitiza changamoto ya kutotumia vipimo vinavyokubalika wakati wa biashara nakusema kwamba vinachangia kushusha tija kwa mazao ya mkulima.
‘Wakulima wanauza kwa kukadiria badala ya kutumia vipimo wengine wanatumia mifuko kukadiria hii inawapunja sana wakulima wetu, alisistiza Bi Katherini
Kwa sasa gharama ya kuzalisha  mazao kama viazi au mahindi kwa ukubwa wa ekari moja ni kati ya sh.719000 mpaka  800,000 kama vipimo havitazingatiwa mkulima hawezi kurudisha gharama au kupata faida alisema Bi Katheri.
Awali wataalamu wa udongo waliwashauri wakulima kote nchini kupima udongo wa mashamba yao kabla ya kuotesha ili kujua madini yanayotakiwa kwenye mbolea badala ya kutumia mbolea kwa kubuni kwani kunachangia kupunguza kiwango cha uzalishaji. 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com