Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki mhe. Miraji Mtaturu amewaomba viongozi wa dini kutojihusisha na siasa ili kutowagawa watanzania bali wabaki katika nafasi ya ushauri ili kuwasaidia wanasiasa kulinda maadili
Mhe. Mtaturu amesema huli katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Sakaa katika kata ya Misughaa tarafa ya Mungaa na amewataka viongozi hao kuendelea kuilinda amani ya watanzania na kutokufuata upepo wa kisiasa kama ambavyo baadhi yao wameanza kutumiwa na wanasiasa.
“Sisi wanasiasa tusifikie mahali tukawafanya hawa viongozi wa dini eti waingie kwenye mchezo wa kisiasa ni kweli siasa na dini unaweza kusema vinaenda pamoja kwasababu watu wote waliopo kwenye siasa wanaimani za dini sasa ukitaka kufanya siasa kama wewe ni kiongozi wa dini unaondoka unakuja kufanya siasa moja kwa moja ukichanganya mambo utawaheruhi waumini hawatamfuata Mungu hawa watafuata mambo ya Kaisali” Mhe. Miraji Mtaturu mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki
0 comments:
Post a Comment