Na Mathias Canal, Bukombe
Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko ameshiriki kupokea Mwenge wa Uhuru ambao leo tarehe 6 Agosti 2023 umewasili wilayani Bukombe ukitokea katika wilaya ya Mbogwe katika Mkoa wa Geita.
Akitoa salamu za ukaribisho amewapongeza viongozi wanaokimbiza mwenge kitaifa kuwa ni watu jasiri wenye uwezo mkubwa wa kutoa hotuba na maelekezo yahusuyo miradi.
Katika Wilaya ya Bukombe Mwenge huo wa Uhuru utakimbizwa umbali wa Kilomita 124 ukiwa umepangiwa kuzindua miradi minne, kuwekwa mawe ya msingi kwenye miradi miwili na kutembelea miradi mitano.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe Said Nkumba akitoa taarifa ya mbio za mwenge amesema kuwa miradi yote itakayozinduliwa, kuwekwa mawe ya msingi na kutembelewa itakuwa na gharama ya Shilingi 1,484,502,732.93
MWISHO
0 comments:
Post a Comment