Naibu wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo,Mhe. Juliana Shonza akijibu swali wakati wa kikao cha tatu
cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo tarehe 5 Septemba 2019 jijini Dodoma.
……………….
Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa Serikali haishikizi
ufadhili katika michezo bali wajibu wake ni kuweka mazingira wezeshi kwa
mfadhili ambaye anataka kufadhili mchezo wowote kutokana na yeye kuona
namna anavyoweza kufaidika katika ufadhili huo.
Mhe.Shonza amesema hayo leo
Bungeni Dodoma alipokuwa anajibu swali la Mbunge Mhe.Sophia Mwakagenda
(Viti Maalum) aliyeuliza Ni lini Serikali itahakikisha ufadhili
unapatikana kwenye michezo inayohusu wanawake hususan michezo ya ngumi.
Akijibu swali hilo Mhe.Shonza
ameeleza kuwa ufadhili wa michezo hutokana na mfadhili kuona faida ya
kibiashara na kijamii wakati anapofadhili ambapo amesititiza kuwa hivi
sasa Tanzania ina ligi kuu ya mpira wa miguu kwa wanawake ambayo
inadhaminiwa na Kampuni ya vinywaji ya Serengeti Breweries kupitia bia
yake ya Serengeti Lite ambayo imefadhili kutokana na faida walioona
itapata.
“Ufadhili haushinikizwi na
Serikali bali ni suala la hiari kwa upande wa wafadhili ambao huchukua
fursa hiyo pale wamapoona fursa za kibiashara zitakazowanufaisha wao,
Hivyo wajibu wa Serikali ni kuimarisha uhusiano na kuweka mazingira
wezeshi ili faida ipatikane kwa pande zote mbili”alisisitiza Mhe.Shonza.
Aidha Mhe. Shonza katika kujibu
swali la nyongeza la mbunge huyo aliyeuliza ni lini Serikali itatoa vifa
vya mazoezi kwa wanamichezo hao, ameeleza kuwa suala la kukuza na
kuendeleza michezo nchini linashirikisha pia wadau hivyo ni wajibu wa
wanachi wote kuona michezo kuwa ni muhimu katika jamii hivyo kuwekeza
katika Nyanja mbalimbali.
Hata hivyo Mhe. Shonza amewaomba
wadau wote wa Michezo nchini kusaidia kushawishi makampuni,Taasisi na
wadau wote kudhamini na kufadhili maendeleo ya michezo nchini ikwemo
wanayoshiriki wanawake.
0 comments:
Post a Comment