Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt
Kheri Kagya akizungumza na wananchi waliojitokeza kufanya mazoezi ya
Viungo katika Uwanja wa Steven Kibona Wilayani Ileje.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela (wa kwanza mwenye kofia nyeusi), akifuatiwa na Mkuu
wa Wilaya ya Momba Juma Said Irando, Mkuu wa Wilaya ya Ileje Jonas Mkude
kisha Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia Opulukwa wakishiriki
mazoezi ya Viungo na wananchi waliojitokeza katika Uwanja wa Steven
Kibona Wilayani Ileje.
Katibu Tawala Wilaya ya Songwe
Johari Samizi (mwenye kofia ya rangi za bendera ya Taifa) akishiriki
mazoezi ya viungo na wananchi waliojitokeza kufanya mazoezi katika
Uwanja wa Steven Kibona Wilayani Ileje.
Wananchi wa Wilaya ya Ileje wakifanya mazoezi ya viungo katika Uwanja wa Steven Kibona Wilayani Ileje.
Wananchi wa Wilaya ya Ileje wakifanya mazoezi ya viungo katika Uwanja wa Steven Kibona Wilayani Ileje.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela akiwapongeza watoto waliojitokeza kushiriki mazoezi
ya Viungo katika Uwanja wa Steven Kibona Wilayani Ileje.
…………………..
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt
Kheri Kagya ametoa rai kwa wananchi wote Mkoani Songwe kuwa na tabia ya
kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kuufanya mwili ubaki na
uzito unaotakiwa na hivyo kupunguza magonjwa yasiyo ambukiza.
Dkt Kagya amesema hayo wakati wa
mazoezi ya Viungo yaliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela katika Wilaya ya Ileje lengo likiwa kuhamasisha
wananchi kujenga mazoea ya kufanya mazoezi mara kwa mara.
Amesema kwa sasa kumekuwa na
ongezeko kwa asilimia 33 la vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza
kama vile shinikizo la damu na kisukari ambavyo hupatikana hasa kwa
kutofanya mazoezi mara kwa mara.
“Mazoezi ni nyenzo muhimu ya
kuzuia magonjwa yasiyoambukiza na inashauriwa angalau kwa siku mtu
ufanye mazoezi kwa dakika 30 na waliojitokeza kufanya mazoezi leo
wasiache kwani watapata maumivu makali na pia hawataweza kuiona faida ya
mazoezi katika afya zao”, amesema Dkt Kagya.
Dkt Kagya ameongeza kuwa miaka ya
1990 vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ambukiza vilikuwa asilimia 19
lakini sasa vifo hivyo vimefikia asilimia 33 na hii imesababishwa na
watu kuacha misingi ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara.
“Ongezeko la vifo vitokanavyo na
magonjwa yasiyo ambukiza linasababishwa na kuacha misingi ya mazoezi,
vitambi sio dili tena, tufanye mazoezi ili kupunguza uzito usiohitajika
kwani kwa sasa tunao watu wengi wenye uzito ulio zidi wastani na
uliopitiliza”, amesisitiza Dkt Kagya
Ameongea kuwa mazoezi ni muhimu
ili kujenga afya bora ya mwili na akili na hasa akina mama wengi ambao
wamekuwa wakihisi kuwa mazoezi ni kwa ajili ya wanaume tu, hivyo basi
wasisubiri matukio bali wafanye mazoezi mara kwa mara kwani afya bora ni
mtaji wa kufikia uchumi wa kati.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig.
Jen. Nicodemus Mwangela amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Songwe hususani
wa Wilaya Ileje waliojitokeza kwa wingi kufanya mazioezi ili kujenga
afya zao.
Brig. Jen. Mwangela amesema
mazoezi hujenga afya bora na uhusiano mzuri hivyo anawapongeza wote
walioshiriki hususani wanawake na watoto walioshiriki kuanzia mwanzo wa
mbio (jogging) mpaka mwisho wapewe hamasa ya kuendelea na mazoezi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Ileje Jonas Mkude amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwa kuhamasisha
wananchi Kufanya mazoezi ili kuboresha afya zao.
Mkude amesema wananchi wa Ileje
wanapenda mazoezi na Michezo hivyo wataendelea kufanya mazoezi mara kwa
mara ili kujenga afya na kukuza michezo Wilayani humo.
0 comments:
Post a Comment