

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah
Kairuki, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa (katikati) na Waziri
wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (kushoto) wakifuatilia hoja
mbalimbali za wafanyabiashara na wawekezaji wakati wa mkutano wa
mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na
wafanyabiashara uliofanyika mkoani Mtwara. Lengo la mkutano huo ni
kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili
wafanyabiashara na wawekezaji hao.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akizungumza wakati wa
mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na
wafanyabiashara uliofanyika mkoani Lindi. Lengo la mkutano huo ni
kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili
wafanyabiashara na wawekezaji hao.

Mbunge wa Mtwara vijijini Hawa Ghasia akichangia jambo wakati
wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji
na wafanyabiashara uliofanyika mkoani Mtwara. Lengo la mkutano huo ni
kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili
wafanyabiashara na wawekezaji hao.

Mfanyabiashara wa matunda mkoani Mtwara Hamis Mfaume akieleza
changamoto zinazomkabili katika biashara yake wakati wa mkutano wa
mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na
wafanyabiashara uliofanyika mkoani humo.

Katibu wa Chama cha Wasioona Mkoani Lindi, Mariam Mfunda
akieleza changamoto wanazokabiliana nazo watu wenye ulemavu katika
shughuli zao za uzalishaji wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya
Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika
mkoani humo.

Meneja wa Usajili wa Walipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Makao Makuu, Rehema Shao akijibu hoja mbalimbali
zilizoibuliwa wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta
binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani Mtwara. (PICHA
ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)
0 comments:
Post a Comment