


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua nguzo za umeme zilizorundikana kwenye kiwanda cha Qwihaya
General Enterprises Company LTD cha Mafinga zikisubiri wanunuzi. Kiwanda
hicho cha nguzo kilitembelewa na Waziri Mkuu, Septemba 26, 2019.
Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Leonard Mahenda, wa tatu
kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Fred Ngwega na wa nne
kusho ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy.

Nguzo za umeme zikiwa kwenye
mtambo wa kuziwekea dawa maalum ya kuzifanya zisishambuliwe na wadudu au
kuungua moto zikiwa katika kiwanda cha Qwihaya General Enterprises
Company Limited cha mjini Mafinga ambacho kilitembelewa na Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa, September 26, 2019

Baadhi ya nguzo za umeme
zilizorundikana zikisubiri wanunuzi kwenye kiwanda cha Qwihaya General
Enterprises Limited cha mjini Mafinga ambacho kilitembelewa na Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa Septemba 26, 2019. {Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment