METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, September 27, 2019

KERO YA MAJI CHANZO CHA SARATANI YA MACHO KWA WATOTO DODOMA




Na Emmanuel Michael Senny

Uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba na miundo mbinu katika huduma za kibingwa kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), umeifanya serikali ya Rais Dk.John Magufuli kuacha alama isiyofutika kwa miongoni kadhaa ijayo.

Moja ya mambo yanayovuta hisia na hamasa ya wagonjwa kujitokeza kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali yanayohusu huduma ya mama na mtoto ni uwepo wa vifaa tiba vya kisasa, vitendanishi na watalaam wabobezi katika idara mbalimbali ikiwamo huduma ya mama na mtoto.

Jana, Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Karim Meshack aliieleza timu ya wanahabari waliofanya ziara ya mafunzo hospitalini hapo kwamba uwekezaji huo ni mkubwa kufanyika katika utawala wa serikali ya awamu ya tano.

Akitoa taarifa kuhusu uwekezaji huo, Karim alieleza: “Kumekuwepo na mafanikio chanya katika utoaji huduma na mpaka sasa imefanya upandikizaji wa figo kwa wagonjwa 7 uliofanyika kwa mafanikio makubwa huduma ambayo awali ilikuwa ikifanyika nje ya nchi.

Zaidi alisema, “Kwa sasa hospitali hiyo ina kitengo cha wagonjwa wa ajali ambacho ni maalumu kwa majeruhi hasa ikizingatiwa Dodoma ni mkoa ulio katikati ya nchi kwa hiyo itakuwa rahisi kuhudumia watanzania kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.”

Kwa mujibu wa sera ya taifa ya afya ya mwaka 1990 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2007, inaeleza kuwa serikali itajielekeza katika mabadiliko ya magonjwa yanayotokea, sayansi na tekonolojia, kwa kuwa serikali inatambua umuhimu wa afya bora kwa wananchi wake kwani afya bora ni rasilimali muhimu kwa maendeleo.

Serikali inafanya maboresho hayo ili kwenda sawa na sera hiyo ili kuzingatia dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025 na  malengo ya milenia.

Pamoja na mambo mengine, serikali inaelezwa kuwekeza rasilimali watu, fedha na miundo mbinu ya kisasa katika  Kitengo cha Kupandikiza Uroto cha Hospitali hiyo ya Benjamin Mkapa ili kukabiliana na ugonjwa wa selimundu.

Mbali na uwekezaji huo, yamo pia matibabu ya kibingwa ya magonjwa ya moyo ambapo mtaalam mbobezi wa magonjwa hayo, Dk. Andrew Kasambala alisema kitengo cha moyo kimepanuliwa na kufanyiwa maboresho makubwa yanayoipa heshima kutokana na shughuli za kibingwa kutoa matokeo yaliyokuwa yakitarajiwa.

Lucy Baraka aliyemleta mama yake hospitalini hapo kwa matibabu ya Miguu akitokea wilayani Gairo Mkoani Morogoro na Kayaya Santa ambao walifika hospitalini hapo kwaajiri ya matibabu wamesifu huduma zinazotolewa hospitalini hapo huku akiiomba Serikali kuboresha huduma katika maeneo mengi zaidi ili kuweza kupata matibabu ya uhakika kwa ukaribu zaidi.

Hospitali hiyo iliyopo kilomita 25 kutoka katika viunga vya Jiji la Dodoma, inafanya upasuaji wa matundu unaotumia vifaa vya kisasa.

Mwisho
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com