Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kampuni ya Engen
inayohusika na uuzaji wa mafuta na vilaini mbalimbali vya vyombo vya moto
ikiwemo magari na pikipiki, imewasogeza karibu huduma wateja wa mikoa ya Kanda
ya Ziwa baada ya kufungua vituo viwili vya mafuta jijini Mwanza.
Ufunguzi wa
vituo hivyo ambavyo ni Engen Sinai pamoja na Engen Mkuyuni umefanyika Septemba
25, 2019 na kutoa fursa kwa wateja kunufaika na ofa mbalimbali ikiwemo mafuta,
jaketi za usalama barabarani, kofia pamoja na tisheti.
Baada ya
kufanya ufunguzi rasmi wa vituo hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Engen
Tanzania, Paul Muhato alisema tayari vituo 10 vya Engen vimefunguliwa katika
mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Arusha na
Dodoma ambapo matarajio ni kuwa na vituo 20 ifikapo mwaka 2020.
Muhato
alisema lengo la kampuni ya Engen ni kuendelea kutoa huduma bora za vilainishi
na mafuta yasiyochakachuliwa kwa wateja wake huku wakiwa na uwanda mpana wa
kufanya malipo kwa mfumo wa taslimu, M-Pesa, kadi za benki pamoja na kadi za
Engen.
Aidha aliongeza
kwamba wateja wa Engen wataendelea kunufaika na ofa na huduma mbalimbali za
bure ikiwemo mteja kusafishiwa gari, kujaziwa upepo pamoja na ushauri wa aina
gani ya vilainishi bora vinafaa gari lake.
Naye Ruben
Petro ambaye ni mmoja wa waendesha bodaboda jijini Mwanza aliyenufaika na ofa
za Engen baada ya ufunguzi wa kituo cha mafuta Engen Mkuyuni, aliishukru
kampuni hiyo kwa kusogeza karibu huduma zake huku ikiwajali kwa ofa mbalimbali
na hivyo kuwasihi wateja wengine kuchangamkia huduma za kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato (kushoto) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo cha mafuta Engen Mkuyuni.
Shangwe na vigeregere baada ya ufunguzi wa kituo cha mafuta Engen Mkuyuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato (kulia) akimjazia mafuta bure mmoja wa waendesha bodaboda jijini Mwanza.
Waendesha bodaboda jijini Mwanza wakinufaika na mafuta bure baada ya ufunguzi rasmi wa kituo cha mafuta cha Engen Mkuyuni jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo cha mafuta Engen Sinai jijini Mwanza.
Shangwe baada ya ufunguzi rasmi wa kituo cha mafuta Engen Sinai jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato (kulia) akimpongeza mmoja wa waendesha bodaboda waliofika katika kituo cha Engen Sinai kunufaika na huduma za Engen.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato (kulia) akimjazia bure mafuta mmoja wa waendesha bodaboda jijini Mwanza baada ya ufunguzi rasmi wa kituo cha Engen Sinai.
Ukifika kituo chochote cha Engen, utanufaika na huduma mbalimbali ikiwemo gari kusafishwa.
0 comments:
Post a Comment