
Na Bashiri Salum ,Mbeya
Wakulima wa viazi na vitunguu
katika kijiji cha Ntangano Ijombe kilichopo Mkoani Mbeya wameiomba
Wizara ya Kilimo kuwasaidia kupata mifuko maalumu itakayotumika kama
Kipimo cha viazi ili kuepuka changamoto ya kujaza mifuko kupoita kiasi
kunakofahamika kama rumbesa
Wakiongea wakati wa mahojiano na
Kitengo cha Mawasiliano mara baada ya kutembelewa shambani kwao hivi
karibuni wamesema mifuko inayotumia kufungashia viazi na vituguu inakuwa
na ujazo mkubwa kuanzia kilo 150 hadi 180 wakati wa kuwapimia
wafanyabiashara .
Aidha wamesema kwamba gharama za
uzalishaji zimekuwa juu hivyo kwa kuuza viazi au vitunguu kwa rumbesa
kunawatia hasara na kushindwa kurudisha gharama za uzalishaji.
Yohana Wilfredi Wangere moja ya
mkulima anayelima mahindi, ngano, viazi na vitunguu katika kijiji
hicho anasema amejenga nyumba kwa kupitia kilimo lakini isingekuwa
changamoto hiyo ya masoko angekuwa amefanya mambo mengine makubwa zaidi.
Bwana Yohana anaendelea kusema
kwamba wamepata changamoto ya ya kununua pembejeo kwa bei ya juu ambazo
hutumika kwa wingi zaid mvua inapokuwa kubwa.
Ameimba serikali kuongeza ruzuku
katika pembejeo ili wakulima hao waweze kuzinunua kwa bei ndogo na
kufanya kilimo chao kuwa na tija.
wizara ya kilimo imeshauriwa kuwa
na ushirikiano mkubwa na mamlaka ya hali ya hewa TMA ili kutoa taarifa
mapema kwa wakulima kuhusu kiwango cha mvua kiatakachokuwepo katika
mikoa ambapo wakulima wajipanga kununa pembejea kulngana na viwango vya
mvua, alisema bwana Yohana.
Akiongea kwa niaaba ya Mrungezi wa
kituo cha utafiti Uyole Bi Katheri Kabungo amesema kwamba kituo cha
utafiti cha uyole TARI UYOE kimekuwa kikitoa msaada mkubwa kwa wakulima
wa maharage, viazi, ngano, pareto na mahindiili lengo likiwa ni
kuongeza tija katika kilimo chao.
akiongea hali soko la wakulima
wa mazao mbalimbali katika mikoa ya nyanda za juu anasema tatizo kubwa
ni tija ndogo inayosababishwa na matumizi yasikuwa sahihi ya viuatilifu,
kutotumia mbolea na mbegu bora za kilimo.
hata hivyo amesisitiza changamoto
ya kutotumia vipimo vinavyokubalika wakati wa biashara nakusema kwamba
vinachangia kushusha tija kwa mazao ya mkulima.
‘Wakulima wanauza kwa kukadiria badala ya kutumia vipimo wengine wanatumia mifuko kukadiria hii inawapunja sana wakulima wetu, alisistiza Bi Katherini
Kwa sasa gharama ya kuzalisha
mazao kama viazi au mahindi kwa ukubwa wa ekari moja ni kati ya
sh.719000 mpaka 800,000 kama vipimo havitazingatiwa mkulima hawezi
kurudisha gharama au kupata faida alisema Bi Katheri.
Awali wataalamu wa udongo
waliwashauri wakulima kote nchini kupima udongo wa mashamba yao kabla ya
kuotesha ili kujua madini yanayotakiwa kwenye mbolea badala ya kutumia
mbolea kwa kubuni kwani kunachangia kupunguza kiwango cha uzalishaji.
0 comments:
Post a Comment