Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha
nne, walimu na wadau wa elimu mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akizindua kambi ya
Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne, waliopata ufaulu hafifu
katika Mtihani wa ‘Mock’ ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa
Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05,
2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akizindua kambi ya Kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha
nne, waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ ili waweze
kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019,
uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha
nne, walimu na wadau wa elimu mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kambi ya
Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne, waliopata ufaulu hafifu
katika Mtihani wa ‘Mock’ ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa
Taifa utakaofanyika Novemba 2019 uzinduzi huu umefanyika Septemba 05,
2019 Mjini Bariadi.
Afisa elimu wa Mkoa wa Simiyu,
Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya kambi maalum ya kitaaluma kwa
wanafunzi waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ wakati wa
ufunguzi wa kambi hiyo inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze
kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019,
uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha
nne, mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi
wa kidato cha nne, waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ ili
waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba
2019 uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu,
Komredi Enock Yakobo akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne
waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ wakati wa ufunguzi wa
kambi hiyo inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza
ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu
umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya walimu mahiri na wadau
wengine wa elimu mkoani Simiyu wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo
inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu katika
mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika
Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Simiyu
ya Mjini Bariadi, Mwl. Paul Susu akieleza umuhimu wa kambi za kitaaluma
wakati wa uzinduzi wa kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha
nne waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ inayofanyika ili
kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa
utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019
Mjini Bariadi.
………………………
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amezindua rasmi kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa
wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu (daraja sifuri)
katika mtihani wa ‘Mock’, lengo likiwa ni kuwasaidia waweze kuongeza
ufaulu wao katika mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Novemba 2019.
Akizindua kambi hiyo Septemba
05, 2019 Mtaka amesema wanafunzi hao watafundishwa masomo manne tu
ambayo ni Kiswahili, Kiingereza ,Uraia(Civics) na Historia, hivyo akatoa
wito kwa walimu mahiri waliochaguliwa kuwafundisha wanafunzi hao kwa
moyo na upendo ili wanafunzi hao waweze kupata alama D na kuendelea
katika mtihani wa Taifa.
“Hawa watoto wafundisheni
masomo manne, Kiswahili, Kiingereza, Historia na Civics; wafundisheni
kwa moyo, wapeni mazoezi ya mara kwa mara katika siku hizi 60
watakazokuwa kambini, muwasaidie watoke kwenye F wapate angalau D nao
wapate vyeti, kwa sababu hata ajira siku hizi kigezo ni angalau mtu awe
na cheti cha kidato cha nne” alisema Mtaka.
Katika hatua nyingine Mtaka
ametoa wito kwa jamii ya Simiyu kuendelea kuwekeza kwenye elimu ili
kuuwezesha mkoa kushindana kiuchumi kwa kuwa maendeleo ya kiuchumi
yanategemea maendeleo ya elimu katika eneo husika.
Afisa Elimu mkoa wa Simiyu,
Mwl.Ernest Hinju amesema kati ya Wanafunzi 9956 waliofanya mtihani wa
Utimilifu (Mock), 1300 hawakupata alama D hata moja, hivyo waliopata
matokeo hafifu (daraja sifuri) wamewekwa pamoja wafundishwe masomo manne
ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa, huku waliopata
daraja la kwanza hadi la nne wakiendelea na kambi kufundishwa masomo
yote.
Aidha, Hinju ameongeza kuwa
kambi za kitaaluma zimechangia kuongeza ufaulu kwenye Mtihani ya Taifa
wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita, ambapo katika
matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ufaulu ulikuwa asilimia 74 mkoa
ukiwa nafasi ya 14 kati ya mikoa 26, mwaka 2017 ufaulu asilimia 79.8
nafasi ya 11 na mwaka 2018 ufaulu asilimia 82.5 ukashika nafasi ya 9
kati ya mikoa 26.
Kwa upande wao wanafunzi wa
kidato cha nne waliopo kambini wameshukuru kuwekewa kambi hiyo na
wakaeleza imani yao juu ya uwepo wa kambi hiyo ambapo wameomba kambi za
kitaaluma Simiyu ziwe endelevu ili ziwasaidie kujifunza na kujiandaa
vema na mitihani ya Taifa hatimaye mkoa uweze kufanya vizuri.
“Tunawashukuru viongozi wetu
na wazazi wetu kwa kukubali kutuwekea kambi ya kitaaluma, ninashauri
kambi hizi zisiishie kwetu ziendelee na kwa wadogo zetu ili mkoa wetu
uweze kuongeza ufaulu” alisema Esther Nashoni mwanafunzi shule ya
sekondari Bariadi(Bariadi)
Mkuu wa Shule ya Sekondari
Simiyu, Mwl.Paul Susu amesema walimu wamejiandaa vema katika
kuwafundisha wanafunzi na kuwapa mitihani ya mara kwa mara ili waweze
kufanya vizuri, huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali wa elimu kujitolea
katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kuwe na miundombinu ya
kutosha itakayoongeza nafasi kwa kambi za kitaaluma kufanyika vizuri.
Kambi ya kitaaluma kwa
wanafunzi wa Kidato cha nne iliyozinduliwa Septemba 05, 2019 ilianza
rasmi Septemba Mosi na inatarajiwa kufanyika ndani ya siku 60 kabla ya
kufanya Mtihani wa Taifa mwezi Novemba.
0 comments:
Post a Comment