Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
amewapongeza viongozi wa dini kwakuwa mstari wa mbele katika kuliombea Taifa na
kuwaomba kuendelea na moyo huo na kukemea vitendo viovu.
Jafo ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika semina ya siku
tatu ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kikiristo mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Jafo amewaomba viongozi hao wa dini kuendelea
kusimamia maadili kwa kuendelea kukemea matendo maovu yakiwemo matumizi ya
madawa ya kulevya, rushwa na mauaji ya vikongwe.
Aidha Jafo amewaomba viongozi hao wa dini kupinga mambo yote
yasiyo mpendeza mungu.
Akizuzungumzia kuhusu amani na utulivu hapa nchini, Jafo amesema
kwasasa nchi inapoelekea katika uchumi wa viwanda ni vyema viongozi hao
wakaendelea kuliombea Taifa kwa kuwa bila amani malengo hayawezi kufikiwa.
Wanasemina wakifuatilia maelekezo katika semina ya siku tatu ya viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Dodoma
0 comments:
Post a Comment