Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo,
Mhandisi Mathew Mtigumwe kushoto kwa niaba ya Wizara akimkabidhi hati ya
makubaliano ya kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya ICRAF mara baada
ya kusaini ya makubalianao ya kushirikiana kulia ni Msimamizi Mkuu wa
Taasisi hiyo Bi. Catherine Muthuri, katika Ofisi za Wizara ya Kilimo
katika eneo la Mtumba, Jijiji Dodoma leo tarehe 16/08/2019
Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo,
Mhandisi Mathew Mtigumwe kwa niaba ya Wizara leo, ametiliana saini ya
makubalianao ya kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa
masuala ya Kilimo Misitu (International Centre for Research in
Agro-Forest – ICRAF). Taasisi ya ICRAF imekwa ikifanya tafiti
zinazolenga kuboresha uhifadhi wa mazingira na uzalishaji wa nishati
jadidifu ambayo ni muhimu katika shughuli za kilimo.
Akizunzungumza baada ya
kusaini hati za makubaliano Katibu Mkuu, Mhandisi Mtigumwe amesema
kimsingi Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo imesahini
makubaliano kwa ajili ya lengo la kushirikiana na ICRAF kwenye maeneo ya
ugunduzi wa misitu inayopatikana kwenye ikolojia maalum, usimamizi wa
misitu kwa lengo la kuongeza tija kwenye eneo hilo.
Mhandisi Mtigumwe ameongeza
kuwa Wizara itashirikiana na ICRAF katika eneo la ufuatiliaji wa madhara
kwenye afya ya udongo, mabadiliko ya tabianchi kwenya ardhi ya kilimo
ili kufanya tafiti zitakazokuja na majibu ya changamoto katika maeneo
hayo.
Mhandisi Mtigumwe ameongeza
kuwa eneo moja la ushirikiano ni kujengeana uwezo wa kitaasisi pamoja na
kubadilishana Wataalam, uzoefu katika tafiti mbalimbali pamoja na
kubadilishana vinasaba vya mimea na mazao ya kilimo na misitu.
Akiongea kwa niaba ya Taasisi
ya ICRAF, Bi. Catherine Muthuri ambaye ni Msimamizi wa Shughuli la
Taasisi hiyo iliyopo Jijini Nairobi amesema Tanzania na Kenya ni
majirani wa muda mrefu na kwamba changamoto zinazowakuta Wakulima wa
Kenya, zinawakuta pia na Wakulima wa Tanzania na kusisitiza kuwa lengo
la nchi hizi mbili ni kuhakikisha mambo mazuri kama ya kushirikiana
katika tafiti; yanafanyika kivitengo kwa lengo la kuboresha Sekta ya
Kilimo.
0 comments:
Post a Comment