Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi wakati akiwa
katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu kukagua utekelezaji wa maagizo ya Waziri
Mkuu aliyoyatoa hivi karibuni kwa wafanyabiashara kununua Pamba ya wakulima, tarehe
6 Agosti 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi wakati akiwa
katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu kukagua utekelezaji wa maagizo ya Waziri
Mkuu aliyoyatoa hivi karibuni kwa wafanyabiashara kununua Pamba ya wakulima, tarehe
6 Agosti 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na
Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani
Simiyu kukagua utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa hivi karibuni
kwa wafanyabiashara kununua Pamba ya wakulima, tarehe 6 Agosti 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Simiyu
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) tarehe 6 Agosti 2019 amefanya ziara ya kikazi mkoani Simiyu
kukagua utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa hivi karibuni kwa
wafanyabiashara kununua Pamba ya wakulima.
Mhe Hasunga ametembelea na
kukagua Kituo cha ununuzi wa Pamba cha Itemelo kilichopo kata ya Dutwa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Kituo cha ununuzi cha Lugulu katika kata ya
Lugulu Wilaya ya Itilima na Kituo cha Kumalija kilichopo katika kata ya Shanwa
wilayani Maswa.
Katika ziara hiyo Mhe
Waziri amejionea hali ya ununuzi wa Pamba ya wakulima ukiwa unaendelea kutokana
na serikali hivi karibuni kupata muarobaini wa mustakabali wa zao hilo.
Waziri huyo wa Kilimo
amepiga marufuku Pamba ya wakulima kupimwa katika mizani zisizofahamika badala
yake lazima ipimwe katika mizani iliyothibitishwa na wakala wa vipimo.
Katika hatua nyingine pia
Mhe Hasunga ametoa kalipio Kali kwa wanunuzi wa Pamba kadhalika vyama vya
ushirika vinavyowakata kilo moja wakulima kwa madai ya mifuko ya kupimia badala
yake ameagiza mkulima akatwe kutokana na uzito wa mfuko sio kukadiria kilo
moja.
Alisema kuwa serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imekusudia
kuwanufaisha wakulima kupitia mazao wanayozalisha kwa kuwaongezea elimu ya
Kilimo bora na chenye tija.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga yupo mkoani Simiyu kwa ajili ya sherehe za wakulima (Nanenane) ambazo
kilele chake ni tarehe 8 Agosti 2019 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga maadhimisho hayo
akimuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment