METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, August 23, 2019

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WATAKA ELIMU ITOLEWE KWA WANANCHI KABLA YA UCHAGUZI MDOGO

Mkurugenzi wa utetezi na maboresho wa mtandao wa haki za binadamu Fulgence Massawe ,akizungumza wakati wa mdahalo ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na kushirikisha baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu na wananchi.
Mkurugenzi wa shirika la Faraja ambalo pia linafanya kazi na watoto wa mitaani  pia ni mchechemuaji wa jamii, Bi.Philipina Labia,akifafanua jambo wakati wa mdahalo ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na kushirikisha baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu na wananchi
Mhadhiri msaidizi wa chuo cha Mtakatifu John,Ntebi Elkana,akichangia mada wakati wa mdahalo ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na kushirikisha baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu na wananchi
Katibu Mkuu klabu ya Haki za Binadamu Chuo cha Mtakatifu John Bw.John Gerald ,akichangia mada wakati wa mdahalo ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na kushirikisha baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu na wananchi
Mwanafunzi kutoka Chuo cha Mtakatifu John,Azimu Ramsey,akiongea wakati wa mdahalo ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na kushirikisha baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu na wananchi
Mwenyekiti klabu ya haki za binadamu Chuo cha Mtakatifu Joh,Bw.Emmanuel Ponda,akielezea jambo wakati wa mdahalo ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na kushirikisha baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu na wananchi
Picha ya pamoja na wanaharakati pamoja na washiriki wa mdahalo ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na kushirikisha baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu na wananchi.

……………
Na.Alex Mathias,Dodoma
Baadhi ya wadau na watetezi wa haki za binadamu wameomba kutolewa kwa elimu ya kutosha kwa wananchi kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni kote hapa nchini.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma wakati wa mdahalo ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na kushirikisha baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu na wananchi.
Wadau hao akiwamo Ntebi Elkana mhadhiri msaidizi wa chuo cha Mtakatifu John, amesema kuna haja  kwa serikali na wadau wengine kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi waelewe ili washiriki katika uchaguzi huo kikamilifu.
“Bado kuna haja ya kutoa elimu ya kutosha kwa watu wajitambue kwa sababu watu wa hali ya chini bado hawajafikiwa na elimu kuhusu huu uchaguzi wa serikali za mitaa ili washiriki kikamilifu” amesema Elkana.
Amesema bado kuna haja ya kutoa elimu ya uraia kwa jamii kwa sababu elimu ya uraia haijawafikia kikamilifu wananchi amebainisha kuna idadi kubwa ya watu hawafikiwi na elimu hiyo.
“Hii elimu ya uraia ifikiwe kwa ukubwa wake sawa tutawafundisha katika vyuo vikuu lakini ukiangalia kuna namba kubwa ya wanaoishia elimu ya chini hawafiki elimu ya juu hii  elimu ya uraia wanaikosa” amesema.
Kwa upande wake Faraja Kikoti ambaye ni mhitimu ya Chuo cha Mtakatifu John, amesema habari na elimu hiyo haiwafikii wananchi wa hali ya chini kwa sababu ya ubovu wa miondombinu maeneo ya vijijini kuna baadhi ya wataalamu hawafiki huko na wananchi kukosa kabisa elimu hiyo.
Nae mkurugenzi wa shirika la Faraja ambalo pia linafanya kazi na watoto wa mitaani ambaye pia ni mchechemuaji wa jamii, Philipina Labia, amesema kuna baadhi ya mashirika ya kiraia yanayopata ruzuku kwa ajiri ya kutoa elimu kwa raia ni wajibu wao kufika hadi ngazi za chini kabisa.
“Haya mashirika yanayopata ruzuku kwa ajiri ya kutoa hii elimu inabidi wafike hadi ngazi za chini kabisa bila kujali kuna vikwazo gani wanakutana navyo, lazima wahimizwe elimu ifike ya kutosha kwa jamii” amesema Philipina.
Amesema bado katiba yetu ina mapungufu na hivyo kuna haja ya kuifanyia mabadiliko kama ambavyo mchakato ulianza amebainisha kuwa bado kuna wananchi hawana elimu ya uraia na hata katiba iliyopo haijawafikia wananchi kiasi cha kujua haki zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa utetezi na maboresho wa mtandao wa haki za binadamu Fulgence Massawe, amesema elimu ya kutosha ipelekwa wa jamii kwani uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu kuliko uchaguzi mkuu.
Kwani viongozi wanaochaguliwa ndio wanaenda kufanya kazi moja kwa moja na wananchi na elimu isipotolewa ya kutosha na  wakachaguliwa viongozi wasiofaa ni hatari kwa jamii hayo kwa sababu itakosa matumaini kabisa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com