Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,
Mhandisi Mathew Mtigumwe anautangazia Umma kuwa, Wizara imeandaa Mkutano
wa Wafanyabiashara wote wa mazao ya nafaka ndani na nje ya nchi.
Walengwa wa mkutano huo ni: – Wasindikaji, Wamiliki wa maghala ya
kuhifadhi nafaka na Wasafirishaji wa nafaka.
Mkutano huo utafanyika kwa muda wa
siku mbili, kuanzia tarehe 29 hadi 30 Agosti, 2019 katika ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Convention Centre
(JNICC), Jijini Dar es salaam kuanzia saa 2:00 Asubuhi.
Ajenda kuu ya mkutano ni kujadili fursa zilizopo kwenye tasnia ya nafaka na jinsi ya kuzitumia ikiwa ni pamoja na masoko.
Mgeni rasmi katika mkutano huo atakuwa, Mheshimiwa, Japhet Hasunga (Mb), Waziri wa Kilimo.
Ili kushiriki Mkutano huo, wasiliana na Wizara ya Kilimo kupitia namba za simu 0744468044/0652424014/0735500220, kupitia baruapepe: ps@kilimo.go.tz au kwa kumwandikia Katibu Mkuu – Wizara ya Kilimo, S.L.P 2182 Dodoma. Thibitisha ushiriki wako kabla ya tarehe 21.08.2019.
Kila mshiriki anaombwa kujigharamia.
0 comments:
Post a Comment