"Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Morogoro tumefurahishwa kuona mijadala na mada zilizowasilishwa kwenye kikao cha SADC ikilenga kuibua mageuzi ya huduma za kiuchumi kama ulivyo mpango mkakati wa serikali ya Awamu tano inayoongozwa na Rais Dk Magufuli" Shaka Hamdu Shaka
"Vyama vya upinzani wakati umefika kuacha kubeza juhudi za serikali kwani kufanya kwao hivyo, kutavifanya vipuuzwe na kuonekana vinaongozwa na watu wenye ufahamu mdogo" Shaka Hamdu Shaka
"SADC licha ya kutoa mwelekeo kwa serikali lakini pia kumevijengea ufahamu vyama vya upinzani vijue changamoto zilizopo na namna ya serikali ya CCM inavyoweka mikakati bila kubahatisha ili kupunguza changamoto zilizopo katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa" Shaka Hamdu Shaka
"Mada na mijadala iliojadiliwa kwa utaalam wa hali ya juu kwenye kikao hicho, takriban ililenga kukuza mbinu za kukuza huduma za jamii, maboresho na uondoaji changamoto katika sekta kama elimu, miundombinu, maji, umeme na kutanua wigo wa biashara" Shaka Hamdu Shaka
"Ni fahari kwa Tanzania kuonekana ikiwa katika reli ya kushughulikia changamoto za kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa wananchi wake, jambo lililowapa mwanga wataalam wabobezi na wasomi wa mataifa mbali mbali Afrika na duniani kwa jumla kusifu na kupongeza hatua mahususi zinazochukuliwa chini ya uongozi wa Rais Magufuli" Shaka Hamdu Shaka
"Matatizo ya kimaendeleo Kusini mwa Afrika kwa jumla wake yamewekewa mkazo huku serikali zake kutakiwa zijiwekee misingi ya ushughulikiaji changamoto na kutafuta ufumbuzi wa haraka na wa kudumu kadri iwezekanavyo" Shaka Hamdu Shaka
"Mkakati wa elimu bora, kanuni za biasahara kikanda, Uzalishaji mali mashambani na viwandani, mawasiliano na usafirishaji yote yamebainishwa sambamba na utatuzi wa shida za maji, barabara, vituo cha afya na wakulima kutopata pembejeo" Shaka Hamdu Shaka
Wakati Tanzania chini ya Serikali za CCM ikichukua juhudi za utatuzi wa changamoto hizo hasa maeneo ya vijijini kwa kupeleka umeme, maji, ujenzi wa barabara na vituo vya afya, ujenzi wa reli za kisasa, ufufuaji umeme wa uhakika wanaobeza juhudi hizo bila vipimo wamefedheheka" Shaka Hamdu Shaka
"Tumefurahishwa kusikia mada na mijadala ikijikita na kuakisi hatua za serikali yetu ambayo imekuwa shamba darasa kwa nchi za Afrika, pia ni somo kwa vyama vya upinzani kujua lipi wakosoe na yepi waunge mkono, vinginevyo viongozi wake watapuuzwa na kuonekana si wenye ufahamu " Shaka Hamdu Shaka
Wakati umefika kwa wataalam waajiriwa katika taasisi za umma, kutimiza wajibu wao na kumsaidia Rais kwa anayoyakusudia pamoja na kuondoa urasimu ili ukamilishaji wa malengo ufikiwe kama ilivyoelekezwa na kutolewa muongozo na ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi" Shaka Hamdu Shaka
"Mijadala na maazimio ya jumla kwa sehemu kubwa yatampa makali zaidi Rais Dk Magufuli kwa yote anayoyakusudia kuyafanya katika serikali yake" Shaka Hamdu Shaka
"Matatizo ya wananchi Kusini mwa Afrika yanahitaji kusimamiwa ipasavyo, matumizi bora ya ardhi, rasilimali na maliasili huku yakipewa kipaumbele ambapo Rais Magufuli ameanza kuonyesha mfano kwenye hili kabla hajakabidhiwa Uenyekiti wa SADC tunazidi kumuombea nako akafanye vyema zaidi' Shaka Hamdu Shaka
Source Majira, Nipashe, la jiji , East Afrika Redio, Planet Redio
0 comments:
Post a Comment