Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia akicheza na watoto wenye mahitaji maalum katika kituo cha
Watoto wenye mahitaji maalum cha shule ya msingi Mbugani, Waziri huyo
yupo mkoani Geita kwa ziara ya siku mbili ya kukagua miradi ya maendeleo
ya sekta ya Elimu
Moja ya majengo hayo
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia William Ole Nasha akikagua maendeleo ya ujenzi wa bweni la
watoto wenye mahitaji maalum katika kituo Maalum cha Shule ya msingi
Mbugani iliyopo mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na watoto wenye mahitaji
maalum (Hawapo Pichani) baada ya kukagua ujenzi wa bweni la Kituo cha
Watoto wenye mahitaji Maalum cha Shule ya msingi Mbugani iliyopo mkoani
Geita.
………………………………………………………..
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa
kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la kisasa la
wanafunzi katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya
msingi Mbugani iliyopo katika halmashauri ya Mji Geita.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha wakati wa ziara ya
kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na wizara mkoani Geita ambapo
amesema fedha hizo zimetolewa ikiwa ni sehemu ya kuboresha elimu
nchini.
Ole Nasha amesema serikali ya Awamu ya Tano inatambua umuhimu wa
kuwajengea fursa na mazingira mazuri ya kusoma watoto wenye mahitaji
maalum na ndio maana imeweka mkazo katika kuhakikisha kwamba
kunapatikana walimu wa kutosha, vifaa vya kufundishia na kujifunzia
pamoja na vitabu ili kuwawezesha kusoma bila vikwazo vyovyote kutokana
na changamoto zao za kimaumbile.
“Kwa miaka mingi jamii nyingi zimekuwa zikiwatenga watoto wenye
mahitaji maalim, lakini kwa sasa nashukuru tumeendelea kuwawezesha
kupata haki yao ya Elimu kama walivyo watoto wengine na kwamba wanaweza
kuwa na changamoto za kimaumbile lakini ubinadamu wao upo palepale
amesema Waziri Ole Nasha.
Amewataka wanafunzi hao wenye mahitaji maalum kutokatishwa tamaa
na changamoto walizonazo za kimaumbile kwani serikali imewawekea
mazingira ya kuwawezesha kufika mbali zaidi katika Elimu na kuwataka
kuendelea kutumia fursa hizo za kielimu ili kutengeneza maisha yao ya
baadaye.
“Wanafunzi, mtu hawezi kujua
kipaji chako ni kipi lakini serikali inakupa fursa ya kuonyesha kipaji
chako, Mhe Rais ametambua uwezo mkubwa wa watu wenye mahitaji maalum na
ndio maana siku hizi tunae Naibu Waziri anayeshughulika na watu wenye
mahitaji maalum ambaye naye ana changmoto ya ulemavu,” amesema Naibu
Waziri.
Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mbugani Edwicka Ndunguru
amemweleza Naibu Waziri kuwa kituo hicho kilijengwa kwa lengo la
kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum kupata haki ya kielimu
katika mazingira wezeshi na kuwapa fursa wengi zaidi wenye mahitaji
maalum wanaoishi mbali na shule zinazotoa elimu maalum kupata elimu.
Amesema mafanikio ya kuwepo kwa vituo vya watoto wenye mahitaji
maalum mbali na kuwawezesha kupata haki yao ya kielimu, pia imewasaidia
kujifunza ujuzi mbalimbali, jamii imetambua nakuthamini umuhimu wa
wanafunzi wenye mahitaji maaluma kupata Elimu na wengine kufanikiwa
kupata kazi katika maeneo mbalimbali.
Wanafunzi wenye mahitaji maalum wanapomaliza hapa wanakua na
ujuzi katika fani za ushonaji, ufumaji na useremala, fani hizi
zimewezesha baadhi kuajiriwa katika maeneo mbalimbali na wengine
kujiajiri amesemu mwalimu Ndunguru.
Kituo hicho chenye vitengo vinne
vyenye jumla ya wanafunzi 143 ambavyo ni vitengo vya ulemavu wa akili,
Viziwi, ulemavu wa viungo na ulemavu wa macho, mbali ya kuhudumia
wanafunzi hao wenye uwezo wa kufika shuleni lakini pia vinahudumia
watoto 38 wenye ulemavu wa kiwango cha juu ambao hawawezi kufika
shuleni.
0 comments:
Post a Comment