Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Ramadhani kailima, (Wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kituo
Kikuu cha Polisi Central (OCS), Kidwadi Karinga (Wa pili kushoto), Mkuu
wa Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko, CP Albert Nyamuhanga (Watatu
kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Kitengo Cha Kushughulikia Malalamiko,
Rabikira Mushi wakiwa katika Kituo Kkuu (Central) kilichopo Wilaya ya
Dodoma Mjini wakiwa kwenye ziara ya Kikazi kituoni hapo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Ramadhani kailima, (Wa kwanza kulia), Mkuu wa Kitengo cha
Kushughulikia Malalamiko, CP Albert Nyamuhanga (Wa pili kulia), Mkuu wa
Upelelezi Mkoa wa Dodoma (RCO), Pipi Kayumba (Wa tatu kushoto), na
Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko, Rabikira Mushi
wakiwa katika kituo cha Polisi Nkuhungu kilichopo Wilaya ya Dodoma
Mjini wakikagua kitabu cha taarifa za Polisi (RB) walipofanya ziara ya
kikazi kituoni hapo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Ramadhani kailima, (Wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kituo
Kikuu cha Polisi Central (OCS), Kidwadi Karinga (Wa pili kushoto), Mkuu
wa Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko, CP Albert Nyamuhanga (Wa tatu
kushoto), wakimsikiliza mwananchi aliyekuwa akisubiri huduma katika
Kituo Kikuu cha Polisi, Wilaya ya Dodoma Mjini wakati viongozi wao
walipofanya ziara ya kikazi kituoni hapo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (Katikati), akitoa maelekezo kwa
viongozi wa Polisi na watendaji wakuu wa Kitengo cha Kushughulikia
Malalamiko baada ya kukamilisha ziara ya kikazi Kituo cha Polisi
Chang’ombe, Wilaya ya Dodoma Mjini. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi)
…………………..
Na Mwandishi Wetu, MOHA
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, amelitaka Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kuboresha mazingira ya huduma wanazotoa kwa wananchi.
Alisema ni wajibu wa jeshi hilo kutoa
elimu kwa jamii iweze kufahamu hatua za kufuata pindi wanapotaka
kuwawekea dhamana ndugu zao waliopo katika vituo vya polisi.
Kailima aliyasema hayo hayo jana alipofanya ziara ya kutembelea vituo vinne vya polisi mkoani Dodoma.
Lengo la ziara hiyo iliyoandaliwa na
Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko Ndani ya Wizara hiyo ni kuangalia
utendaji kazi wa jeshi hilo juu ya huduma wanazotoa kwa wananchi.
Vituo alivyotembelea ni vile vilivyopo katika Wilaya ya Dodoma Mjini ambavyo ni Kituo Kikuu (Central), Chang’ombe, Nkuhungu na Kikosi cha Usalama Barabarani.
Katika ziara hiyo, Kailima aliambatana na
Mkurugenzi wa Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko, Kamishna wa Polisi,
Albert Nyamuhanga pamoja na Maafisa wengine wa kitengo hicho.
Akiwa kwenye kituo Kikuu cha Polisi
(Central), Kailima alikuta idadi kubwa ya watu waliokuwa na shida
mbalimbali, alitumia fursa hiyo kuzungumza nao na kuwataka waeleze kero
zao.
Baada ya kuzungumza na wananchi, Kailima
aliushauri uongozi wa kituo hicho kuweka mazingira mazuri ya kutoa
huduma ili kuondoa mrundikano wa wananchi nje, ndani ya kituo.
“Wekeni mazingira mazuri ya mwananchi
mmoja kuhudumiwa na askari mmoja kutokana na idadi ya askari ambao
watakuwa zamu ili kupunguza msongamano,” alishauri.
Aliongeza kuwa; “Toeni elimu inayohusu
dhamana kwa jamii ili wananchi wajipange kabla ya kuja kituoni, unakuta
watu wengi wanakuja kuwawekea dhamana ndugu zao bila kujua taratibu
hivyo kusababisha wajazane kituoni bila sababu,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Mkuu wa Upelelezi Wilaya
ya Dodoma, Pipi Kayumba, alisema katika utendaji kazi wake, kila siku
anapita kituoni hapo ili kuonana na wananchi anaowakuta kituoni,
kusikiliza shida zao.
Alishauri ili jeshi hilo liweze kuboresha
huduma zake, kuwepo vituo vya polisi katika njia zote za kuingia jijini
Dodoma kwani jiji hilo limekuwa kubwa, idadi ya watu imeongezeka.
“Kwa sababu ya ongezeko kubwa la watu,
hata utoaji huduma nao umekuwa mkubwa, kuanzishwa kwa vituo hivyo
litakuwa jambo jema kwa Jeshi la Polisi na nchi kwa ujumla,” alisema.
Kwa upande wake, Kamishna Nyamuhanga
alishauri Mkuu wa Kituo hicho, Kidwadi Karinga, aweke mkakati wa kuondoa
malalamiko ya wananchi kwenye kituo hicho.
Kailima aliendelea na ziara yake kwenye
Kituo cha Kikosi cha Usalama Barabarani, kuzungumza na wananchi waliodai
kuna mtu ambaye si askari alikuwa akitoa taarifa ya upotevu wa mali
(loss report).
Mtu huyo alikuwa akitoa taarifa hiyo nje
ya kituo hicho kwa gharama kubwa wakati gharama halisi ni sh. 500 tu,
hulipwa kwa utaratibu uliowekwa na kupewa lisiti.
Kailima alitumia fursa hiyo kuwaeleza
wananchi kuwa lengo la ziara hiyo ni kujionea mazingira ya kazi za
askari kwa jamii ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.
Alimpongeza Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Nuru
Selemani kwa kutekeleza agizo la Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola
juu ya kuziondoa pikipiki zilizokamatwa kwa makosa mbalimbali.
“Wasisitize askari wako waache kuomba na
kupokea rushwa, kutobambika kesi kwa wananchi, askari kutumia lugha
nzuri, kuelimisha wananchi wanapofanya kosa, kutoa elimu katika redio
namna ya kuvuka kwenye zebra, kutoa taarifa kuhusu hali ya mji kila
siku,” alisisitiza Kailima.
Aliwataka askari wa Usalama Barabarani
wafanye operation kubwa mara moja kwa mwezi ili kufanya wepesi wa
kukusanya maduhuli ya serikali, kutimiza wajibu wao wawapo kazini na
wanaokwenda tofauti wachukuliwe hatua stahiki.
Alisisitiza suala la usalama hasa kipindi
hiki ambacho kuna ugeni wa Mkutano wa SADC kuanzia Agosti 5, mwaka huu,
hivyo kama chombo cha usalama wamuunge mkono Rais Dkt. John Magufuli.
Pia Kailima alitembelea Kituo cha
Chang’ombe kinachohudumia kata tatu za Chamwino, Chang’ombe na
Chinangali ambapo hali ya usalama si nzuri kutokana na matukio ya wizi,
unyang’anyi.
Matukio hayo yamelifanya jeshi hilo kufanya msako mkali na tayari baadhi ya watuhumiwa wamefikishwa mahakamani.
Kailima aliushaurio uongozi wa kituo hicho na askari kuitumia jamii au serikali za mitaa ili kupata taarifa za wahalifu.
Mkuu wa kituo hicho, Emanuel Mawi,
alisema kuna doria inafanyika maeneo mbalimbali, pia wanashirikiana na
jamii, changamoto waliyonayo ni udogo wa kituo ambacho kinahudumia eneo
kubwa.
Akiwa kwenye Kituo cha Nkuhunga, Kailima aliambiwa kituo hicho kinahudumia kata mbili za Nkuhungu na Kizota.
Akiwa kituoni hapo, Kialima aliambiwa kituo hakilazi mahabusu ambao hupelekwa Kituo Kikuu (Central).
Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Dodoma, Kayumba alisema changamoto waliyonayo ni uchache wa magari kwa ajili ya doria za kila siku.
Kailima aliwapongeza Kayumba na Karinga kwa kazi kubwa wanayoifanya.
Kwa upande wake, Kamishna Nyamuhanga,
alimshukuru Kailima na kumuahidi kuwa, watatekeleza maelekezo yote
aliyotoa katika ziara hiyo ili kuboresha utendaji kazi.
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki zoezi la upandaji wa mbegu za pamba kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya mji wa Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,akiwasili kwenye eneo la shamba na kusalimiana na viongozi wa halmashauri hiyo akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi.
Afisa Kilimo wa halmashauri ya mji,Bw Samwel Ng'wandu akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga.
Baadhi ya watumishi na Jeshi la akiba (MGAMBO)wakishiriki shughuli za kupanda mbegu kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya mji.
NA JOEL MADUKA,GEITA
Wataalamu wa kilimo mkoani Geita wametakiwa kuwafuatilia kwa karibu wakulima wa pamba na kuwaelekeza kulima kwa tija ili kuzalisha zaidi tofauti na miaka ya nyuma.
Akizindua msimu wa kilimo cha pamba kwenye mashamba ya watumishi wa Halmashauri ya mji wa Geita yaliyoko kata ya Buhalahala ,Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema ni vema wataalam hao wakafika kwenye maeneo ya kilimo na kuwaelekeza wakulima kanuni zitakazowasaidia kuvuna pamba nyingi.
“Wito wangu kwa wakulima wote pamoja na wataalam wetu wa kilimo baada ya uzinduzi huu mkubwa kabisa wa kilimo cha pamba Mkoani kwetu,wataalam ni vyema wakawasaidia wakulima kufuata zile kanuni kumi bora za kilimo ambacho kitaweza kuwa saidia wakulima lakini nataka twende kisayansi zaidi”Alisema Luhumbi.
Mhandisi Luhumbi Aliongezea Kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kumsaidia mkulima na kuwataka wakulima kuchangamkia fursa hiyo na kuwekeza katika sekta ya kilimo cha pamba kwa kuwa hali ya hewa ya mwaka huu ni nzuri.
Mshahuri wa kilimo cha Mkataba Mkoani Geita Bw Joshua Mirumbe alisema lengo ni kuhakikisha wanaongeza tija ya uzalishaji kutoka wastani wa kilo 250 hadi 300 na kwenda kwa wastani wa kilo 800.
Katika msimu wa mwaka 2016/2017 mkoa wa Geita ulilenga kulima hekta 67002 zilizotarajiwa kuzalisha tani ,93437 za pamba lakini utekelezaji ulikuwa hekta 24 791 zilizozalisha tani 13 267.8 zenye thamani ya Sh Bilioni 15.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki zoezi la upandaji wa mbegu za pamba kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya ...
0 comments:
Post a Comment