Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na mgeni
wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kabla ya kuanza
mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na mgeni wake
Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mara baada ya
kubadilishana zawadi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya
pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli akiongoza ujumbe wa Tanzania
katika mazungumzo ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril
Ramaphosa pamoja naujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa
Jamhuri ya AfrikaKusini Cyril Ramaphosa wakati wakizungumza na
waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Jamhuri
ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mara baada ya kumaliza kikao chao na
Waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
RAIS Dkt. John Magufuli amesema
Tanzania itazidi kufungua milango ya ushirikiano na Jamhuri ya Afrika
Kusini na kuwataka Wafanyabiashara na Wawekezaji wa nchi hizo kutumia
fursa za vivutio mbalimbali vilivyopo ili kukuza uchumi kwa manufaa ya
wananchi wa Mataifa hayo.
Akizungumza leo Alhamisi (Agosti
15, 2019) Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wa mazungumzo yake na Rais
wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, Rais Magufuli alisema
Tanzania na Afrika Kusini ni mataifa rafiki yenye historia ya
ushirikiano katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Aliongeza kuwa Jamhuri ya Afrika
Kusini ni miongoni mwa Mataifa yaliyopiga hatua kubwa za maendeleo ya
kiuchumi katika Bara la Afrika, hivyo Tanzania itatumia fursa hiyo na
mshirika wa karibu kwa ajili ya kupanua wigo wa sekta za kibiashara
ikiwemo ununuzi na uuzaji wa bidhaa na mazao mbalimbali.
“Katika Nchi za SADC, mwaka 2018
Tanzania imeongoza katika ukanda wa SADC kwa thamani ya mauzo ya bidhaa
zake Nchi ya Afrika Kusini iliyofikia thamani Dola Milioni 742.02, na
biashara baina ya Mataifa haya ilifikia thamani ya Dola Bilioni 1.18
kutoka Dola Bilioni 1.11 mwaka 2017” alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli alitoa wito
kwa Wafanyabiashara na wawekezaji wa Afrika Kusni kuja kwa wingi nchini
kwa ajili ya kuwekeza na kufanya biashara kwa kuwa Serikali imeendelea
kuimarisha na kuweka mazingira wezeshi ikiwemo ujenzi wa miundombionu ya
uhakika, pamoja na uimarishaji wa mifumo ya kitaasisi katika usimamizi
wa kodi na biashara.
Akifafanua zaidi Rais Magufuli
alisema Tanzania imejipanga kikamilifu katika kuimarisha mfumo imara wa
uchumi wake ikiwemo kupitia ujenzi wa viwanda, ambayo ndiyo Dira na
dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tanzania katika kufikia uchumi wa kati
ifikapo mwaka 2025, hivyo aliwataka wawekezaji wa Afrika Kusini kuja
nchini na kujenga viwand.
“Katika Bajeti ya Serikali kwa
mwaka tunatenga kiasi cha Tsh Bilioni 270 kwa ajili ya ununuzi wa madawa
nje ya nchi, tunawaomba wawekezaji wa Afrika Kusini waje Tanzania
wajenge viwanda vya madawa kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumepunguza
gharama kubwa za uagizaji wa madawa kutoka nchi ya nchi” alisema Rais
Magufuli.
Akifafanua zaidi Rais Magufuli
alisema Serikali imekusudia miundombinu ya usafiri wa reli Tazara ili
kuweza kutumika na Wafanyabiashara wa Afrika Kusini kwa ajili ya
usafirishaji wa bidhaa mbalimbali pamoja na kutangaza fursa za vivutio
vya utalii na fukwe za bahari zenye urefu wa takribani Kilometa 1400
zilizopo nchini.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli
alisema Tanzania ipo tayari kufanya biashara na Jamhuri ya Afrika Kusini
ikiwemo ununuzi wa vifaa mbalimbali ikiwemo magari, ambayo Tanzania
imekuwa ikiyanunua katika nchi za mbali, huku akitolea mfano wa pikipiki
zinazotumika katika Mkutano wa 39 wa SADC zimenunuliwa kutoka nchini
Afrika Kusini.
Kwa upande wake Rais Cyril
Ramaphosa alisema ziara yake nchini Tanzania ni kielelezo cha kuendelea
kuimarika kwa ushirikiano baina ya Mataifa hayo na kusema Serikali yake
itaweka mazingira wezeshi kwa Wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania
kwenda nchini Afrika Kusini kufanya biashara na kutafuta fursa ya maeneo
ya uwekezaji na biashara.
Aliongeza kuwa Serikali yake
inatambua umuhimu wa sekta ya biashara na uwekezaji katika kukuza uchumi
katika Nchi za SADC kupitia ajenda ya Maendeleo Endelevu ya jumuiya
hiyo ya mwaka 2030 ambayo imedhamiria katika kujenga mazingira bora ya
biashara katika Jumuiya hiyo.
0 comments:
Post a Comment