Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Eng.
Mathew Mtigumwe akiongoza kikao cha pamoja katika ya Wataalam kutoka
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA pamoja na Idara ya Usalama wa
Chakula walipokuwa wakiteta na Ugeni kutoka Shirika la Mpango wa
Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) ukiongozwa na Bi. Miriam Van Den Bergh
na Riaz Lodhi
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Eng.
Mathew Mtigumwe akiongoza kikao hicho kushoto kwake ni Eng. Imani
Zobonaliba na Bwana Ally Mohamed kutoka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula (NFRA)
Ugeni kutoka Shirika la Mpango wa
Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) kutoka kushoto ni Bi. Nima Sitta
Mwakilishai wa WFP Ofisi ya Dodoma, Bi. Miriam Van Den Bergh Msimamizi
Mkuu wa Ununuzi wa Mazao ya Chakula Afrika, Riaz Lodhi, Mkuu wa Kitengo
cha Manunuzi na Mnyororo wa Thamani wa Mazao Tanzania na wa mwisho ni
Bi. Wambui Mbugua Msimamizi wa Manunuzi ya Mazao Kenya
…………………….
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Eng.
Mathew Mtigumwe amewahamasisha Wakulima wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa kuanza
kulima mtama mweupe kwa wingi kwani tayari kuna soko la uhakika kutoka
kwa Shirika la Mpango la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP).
Eng. Mtigumwe ameyasema hayo
wakati wa mazungumzo yake na ugeni kutoka Ofisi ya WFP Kanda ya Afrika,
ugeni uliotokea Jijini, Nairobi nchini, Kenya ukiongozwa na Bi. Miriam
Van De Bergh ambaye ndiye Msimamizi Mkuu wa Ununuzi wa Mazao ya Chakula
Afrika.
Eng. Mtigumwe amesema ugeni huo
umemuhakikishia kuwa Wakulima wa mahindi wa Tanzania kuwa wataendelea
kunufaika na uwepo wa Shirika hilo lakini pia wametoa fursa ya kununua
mtama mweupe kutoka katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kuwa hali ya hewa
inaruhusu zao hilo kulimwa lakini pia itakuwa rahisi kwa Shirika hilo
kusafirisha shehena ya zao hilo baada ya kuvunwa.
Akiongelea hali ilivyo ya fursa
mpya ya kununua mtama mweupe Bwana Riaz Lodhi, Mkuu wa Kitengo cha
Manunuzi na Mnyororo wa Thamani wa Mazao Tanzania amesema WFP imeichagua
Tanzania kuwa sehemu ya eneo la kununua mtama mweupe kwa kuzingatia
vigezo vingi kama; hali ya hewa, mahusianao ya muda mrefu ya kibiashara
pamoja na nguvu kazi iliyopo.
Bwana Liaz ameongeza kuwa mwaka
jana pekee WFP ilinunua kiasi cha tani elfu 80 (80,000) za mtama mweupe
kutoka nchi za jirani na kusafirisha shehena hiyo hadi Sudan Kusini.
“Tumeona ni vyema tuilete fursa
hii kwa Tanzania na Katibu Mkuu naomba utufikishie ujumbe huu kwa
Wakulima wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kuchangamkia fursa hii ya kulima
mtama mweupe, sisi tutaununua kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula NFRA na kupeleka kwenye maeneo yenye uhitaji kama Sudani
Kusini”. Amekaririwa Bwana Liaz.
Kwa upende wake Eng. Mtigumwe
amesema kwa kuanzia Wizara itawahamasisha Wakulima kuanza kulima zao
hilo kwa wingi lakini pia atatoa maelekezo kwa Taasisi ya Utafiti ya
Kilimo (TARI – Ukiliguru) kutoa elimu na aina bora za mbegu za mtama
mweupe kwa ajili ya kuwapa Wakulima.
“Nitawaita Taasisi yetu ya Utafiti
wa Kilimo (TARI) ili tuweke mazingira mazuri ya kuchangamkia fursa hii
ya kulima zao la mtama mweupe kwa Wakulima wetu wa mikoa ya Kanda ya
Ziwa”. Amekaririwa Katibu Mkuu, Eng. Mtigumwe.
0 comments:
Post a Comment