Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI Selemani Jafo leo hii Agoust 16 amemaliza mgogoro wa wanafunzi
uliokuwa umeota sura mbaya ya kuhatarisha hali ya amani shuleni hapo
ambapo mgogoro huo ulianza tangu Augost 10 mwaka huu. Waziri huyo wa
TAMISEMI alitoa onyo kwa walimu ambao inaonekana wameshindwa majukumu
yao ya kiuongozi hadi shule kuingia katika mapigano makubwa kati ya
kidato cha tano na kidato cha sita pamoja na kuchipuka kwa tofauti za
mitazamo ya kidini shuleni hapo.
Wanafunzi na walimu wa shule hiyo wamemshukuru sana waziri huyo kwani walikiri kwamba uhasama shuleni hapo ulikuwa mkubwa sana.
Waziri huyo alifanikiwa kuongea na
kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiwa pamoja na kamati ya Wilaya ya
Moshi,Bodi ya shule wakiwa pamoja na walimu wote wa shule hiyo, na
kuhitimisha na kikao cha wanafunzi.
Jafo alimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Anna Ngwila kuendelea kufanya uchunguzi wa waanzilishi wa
chokochoko hizo ili watakao bainika wachukuliwe hatua za kinidhamu.
Aidha,Jafo alimaliza ziara hiyo
shuleni hapo kwa kuunda timu kumi zenye mchanganyiko mbalimbali ambazo
zitashindana katika michezo mbalimbali na kuzipa majina ya
Tanzanite,Gold,Diamond,Kilimanjaro, Manyara,Serengeti,Ngorongoro,Mikumi,
Nyerere Park, na Ruaha kitendo ambacho kilisababisha shangwe kubwa kwa
wanafunzi hao
0 comments:
Post a Comment