Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulika na Afya Dkt.
Dorothy Gwajima akiongea na Wanganga Wakuu wa Mikoa, Waratibu wa Mtua
ngazi ya Halmashauri, Waratibu wa Ukimwi na watumishi wa vituo vya
kutolea Huduma za afya wanaofadhiliwa na Mfuko wa” Global Fund” wakati
akifunga kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa
Dunia wa kupambana na ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria kilichofanyika
katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango , Jijini Dodoma.
Baadhi Waganga Wakuu wa Mikoa,
Waratibu wa Mtua ngazi ya Halmashauri, Waratibu wa Ukimwi na watumishi
wa vituo vya kutolea Huduma za afya wanaofadhiliwa na Mfuko wa” Global
Fund” wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt. Dorothy Gwajima,Wakati
akifunga kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa
Dunia wa kupambana na ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria kilichofanyika
katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango , Jijini Dodoma.
Mratibu wa Mfuko wa Dunia wa
kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria Dkt. Athumani Pembe kutoka
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa akiongea Waganga
Wakuu wa Mikoa, Waratibu wa Mtua ngazi ya Halmashauri, Waratibu wa
Ukimwi na watumishi wa vituo vya kutolea Huduma za afya wanaofadhiliwa
na Mfuko wa” Global Fund” Wakati kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa
shughuli za Mfuko wa Dunia wa kupambana na ukimwi, Kifua Kikuu na
Malaria kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango ,
Jijini Dodoma
………………………
Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt. Dorothy
Gwajima amewaagiza waratibu wote wa miradi ya Afya chini ya Mfuko wa
Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria kusimamia
utekelezaji kwa weledi ili kuhakikisha walengwa wanapata huduma bora kwa
wakati na kuongeza kasi ya kudhibiti magonjwa haya kwa Kinga na Tiba.
Ameyasema hayo leo wakati akifunga
kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Dunia wa
Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria kilichofanyika katika Ukumbi
wa Mikutano wa Chuo cha Mipango , Jijini Dodoma
Amesema kuwa, Vita dhidi ya
magonjwa haya itafanikiwa zaidi iwapo kila mmoja atawajibika katika
nafasi yake na kuhakikisha shughuli zilizopangwa zinatekelezwa kwa
wakati na ufanisi na taarifa husika zinatolewa kwa wakati na ubora.
Dkt. Gwajima amesema, viongozi
wote ngazi ya Halmashauri wahusike na utekelezaji wa miradi hii kwa
kuwa, siyo suala la wataalamu wa afya pekee bali sekta zote wakiwemo
Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Mipango wa Halmashauri na Waweka
Hazina wa Halmashuari.
Amesisitiza kuwa, katika safari ya
kuelekea kwenye nchi ya viwanda na uchumi wa kati, sekta ya afya ni
mdau mkubwa kwa kuwa, kadri wananchi wenye uhitaji wanavyopata huduma
bora za afya kwa wakati na kadri wanavyoepuka maradhi ndivyo
wanavyoongeza kasi ya safari hiyo hivyo, kila anayeshindwa kuongeza kasi
ya utekelezaji wa miradi hiyo anapunguza kasi ya safari hiyo na
atachukuliwa hatua.
Dkt. Gwajima amezipongeza
halmashauri 85 ambazo zimefanya vizuri kwenye utekelezaji wa mradi huo
kwa kasi kubwa na amezitumia salaam halmashauri zingine 100 ambazo
zimesuasua kwenye utekelezaji wa miradi hiyo na kuwataka kuandaa
maelezo ya kutosha kwa nini wasihesabiwe kuwa wanakwamisha safari ya
nchi kwenda kwenye viwanda na uchumi wa kati kwa kuchelewesha huduma.
“Nimesikitishwa na Baadhi ya
Halmashauri nchini ambazo zina kasi ndogo ya kutekeleza miradi hii na
ninachokiona hapa ni uzembe tu ambao itabidi wahusika wawajibike, kwa
nini wengine watekeleze kwa wakati na ufanisi wengine wabaki nyuma”
Amehoji Dkt. Gwajima
Wakati huohuo, amewaagiza Waganga
Wakuu wa Mikoa na Wilaya na Waratibu wote wa Miradi hiyo kuwa, wakumbuke
nafasi walizonazo ni kama ibada kwa kuwa, zinahusisha masuala ya uhai
na uponyaji hivyo, wasimamie kikamilifu utekelezaji wake na
kuwashirikisha viongozi wote na kufanya kazi kwa ushirikiano ili
kuunganisha nguvu katika kukabiliana na changamoto za utekelezaji.
Aidha amewahimiza kuwasilisha taarifa za utekelezaji zikiwemo stakabadhi za kukiri mapokezi ya fedha kwa wakati.
0 comments:
Post a Comment