Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.
Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimsikiliza Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi
wa Hifadhi, M. B. Moronda mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika
Hifadhi ya Taifa Ibanda wilayani Kyerwa katika mwambao wa mto Kagera
mpakani mwa Tanzania na Uganda. Katikati ni Kamishna Mwandamizi wa
Uhifadhi Kanda ya Magharibi , Martin Loibooki.
Wahifadhi wakiwa na Waziri wa
Maliasili na Utalii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika Orugundu
wilayani Karagwe wakati wa ziara ya Kikazi ya Waziri wa Maliasili na
Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla katika hifadhi hiyo.
************
Na. Aron Msigwa – WMU
13/7/2019. Kagera.
Serikali imesema itawapandikiza Sokwemtu katika hifadhi ya Taifa ya Rumanyika Orugundu iliyoko wilayani Karagwe na Ibanda iliyoko Kyerwa, mkoani Kagera kwa kuwa hifadhi hizo zina Ikolojia na chakula cha kutosha kinachoruhusu kustawi kwa wanyamapori hao hatua itakayochangia kukuza shughuli za utalii wa Sokwemtu hapa nchini na kuongeza pato la Taifa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa
kauli hiyo mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya Kikazi ya kukagua
maendeleo ya shughuli za uhifadhi katika hifadhi hizo zilizotangazwa
hivi karibuni kuwa hifadhi za Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Dkt. Kigwangalla amesema mpango huo umekuja kufuatia taarifa za
kitaalam zinaonesha kwamba katika miaka mingi iliyopita kulikua na
Sokwemtu katika maeneo hayo ya wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambayo
watalaam wanasema ikolojia yake inaruhusu kustawi kwa wanyamapori hao
kwa kuwa yana makazi mazuri na chakula cha kutosha.Amesema mpango huo hautahusisha upandikizaji wa wanyamapori
0 comments:
Post a Comment