
Mkurugenzi wa Shirika la Reli
(TRC) Bw. Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari hukusu
reli ya zamani ya shirika hilo ambayo itafungwa kwa saa 72 kwa ajili ya
ukarabati katika banda la shirika hilo kwenye maonesho ya biashara ya
Sabasaba barabara ya Kirwa jijini Dar es Salaam leo.

………………………………………..
Na Grace Semfuko,MAELEZO
Shirika la Reli Tanzania TRC
limeanza kukarabati njia ya Reli ya kati ya kutoka Dar Es Salaam mpaka
Isaka iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga takribani kilomita 970
ili kuimarisha reli hiyo yenye kiwango cha Mitagauge zoezi ambalo
lilianza Juni mwaka huu na kutarajia kukamilika mwaka 2020.
Katika Utakabati huo Shirika hilo
linatarajia kufunga njia za reli hiyo kwa saa 72 kwa wiki ikiwa ni sawa
na siku tatu kwa Wiki kwa muda wa miezi mitano kuanzia Julai hadi
Novemba 2019, zoezi zoezi ambalo kukamilika kwake kutaingiza faida mara
dufu ya usafiri huo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
wa Shirika hilo Masanja Kadogosa wakati akizungumza na Waandishi wa
Habari kwenye viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba
Jijini Dar Es Salaam na kubainisha kuwa kukamilika kwa Reli hiyo
kutaongeza mapato ya usafirishaji wa Reli kwa asilimia mia moja.
“Waandishi wa Habari na
Watanzania kwa ujumla, TRC sasa tunakuja kuimarisha miundombinu yenu ya
Reli, tunafanya hivi kwa kuwa tunafahamu mnahitaji huduma hizi, tunaomba
mtuvumilie kwa siku ambazo tutafunga njia hizi”alisema Kadogosa.
Alisema kwa treni za kawaida za
mjini (Cummuter Train) za kutoka Kamata kwenda Ubungo na Pugu zitafanya
kazi siku za jumatatu hadi Ijumaa huku Treni za kawaida (Ordinary Train)
za kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma, Mwanza na Mpanda zitafanya kazi
siku za Jumatatu na Jumatano saa tisa alasiri tu na treni za Deluxe ya
kutoka Dar kwenda Kigoma zitakuwepo siku ya Jumanne pekee.
Alibainisha kuwa ukarabati
mwingine wa njia ya Reli kutoka Tanga kwenda Arusha ulianza mapema
mwaka huu ambapo njia hiyo itaanza kutumika mwezi Desemba mwaka huu.
“Ndugu zangu wa mikoa ya
Kaskazini mtaanza kunufaika na usafiri wa treni ya Abiria kuanzia
Desemba mwaka huu, yaani Sikukuu zaKrismas na Mwaka mpya mtaenda
nyumbani na Treni ya Abiria ya TRCälisema Kadogosa.
Akizungumzia ujenzi wa Reli ya
Standard Gauge inayoendelea kujengwa Nchini Kadogosa alisema kwa awamu
ya kwanza kutoka Dar Es Salaam kwenda Morogoro ujenzi huo umefikia
asilimia 56.
0 comments:
Post a Comment