Katibu Mkuu mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu
Bw. Mussa Uledi akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo
waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika
kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini
mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 9, 2019 ikiwa
ni siku ya pili ya mafunzo hayo yaliyofunguliwa Julai 8, 2019 na Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya
kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao
kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 9,
2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo yaliyofunguliwa Julai 8,
2019 na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana
Shonza.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari-
MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya
kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao
kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo
Julai 9, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo yaliyofunguliwa
Julai 8, 2019 na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Juliana Shonza.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya
kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao
kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo
Julai 9, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo Bi Nelly Mtema
akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyofunguliwa Julai 8, 2019
na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana
Shonza..
(Picha zote na Abubakari Kafumba, MAELEZO- Morogoro)
…………………
Na Frank Mvungi- MAELEZO- Morogoro
Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu,
Bw. Mussa Uledi amesema kuwa Tanzania inanufaika kiuchumi kama
mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na
jumuiya nyingine ambazo Tanzania ni mwanachama.
Akizungumza wakati akiwasilisha mada leo
mjini Morogoro ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi wa habari
ya kuwajengea uwezo wa kuandika na kuripoti habari za SADC, Bw. Uledi
amesema kuwa nchi yetu imenufaika na utekelezaji wa miradi ya
miundomnbinu, biashara, uwekezaji na viwanda.
“ Mkakati wa maendeleo wa SADC
unafafanana kwa kiwango kikubwa na ule wa Tanzania ambao pia unazingatia
haja ya utekelezaji wa viwanda na miundombinu hapa nchini hali
itakayochangia katika kuimarisha maendeleo na kukuza uchuni na ustawi wa
wananchi” Alisisitiza Bw. Uledi
Akifafanua amesema kuwa vipaumbele vya
Tanzania vimejikita katika upanuzi wa Mauzo nje na uongezaji wa michepuo
yake lengo likiwa ni kukuza na kuendeleza biashara hali inayowezesha
uendelezaji wa viwanda vya kuongeza thamani katika malighafi za ndani
hususan mazao ya kilimo na madini.
Aliongeza kuwa ziara ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli katika baadhi ya nchi
wanachama wa SADC imeonesha kuwa Tanzania imejipanga vizuri kimkakati
inaweza kuwa ghala la Chakula kwa kukuza zaidi uzalishaji kuendana na
mahitaji katika soko la jumuiya hiyo na hata nje ya jumuiya.
Alitaja vipaumbele vingine kuwa ni
pamoja na uendelezaji miundombinu kama barabara, reli, usafiri wa anga,
uzalishaji na usambazaji huduma za umeme ambayo ni nyenzo muhimu sana
katika kuyaunganisha masoko ya nchi wanachama wa SADC.
Aliongeza kuwa vipaumbele vingine ni
utafutaji wa rasilimali na utekelezaji wa miradi ya Kikanda kwa kuundwa
kwa kikosi kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya Fedha na uendelezaji
miundombinu, Amani na Usalama umeendelea kuimarika ndani ya SADC.
Tanzania inatarajiwa kuleta msukumo mpya
kwa nchi wanachama wa SADC katika utekelezaji wa miradi na program za
maendeleo za Jumuiya hiyo kwa kuwa itakuwa na dhamana kubwa ya kukidhi
matarajio makubwa ya nchi wanachama wakati wote wa uenyekiti wake.
Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni na
Mafunzo, Brigedi ya Magharibi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) Kanali Wilbert Ibuge akiwasilisha mada katika mafunzo
hayo amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa Barani
Afrika zilizotoa mchango mkubwa na kuratibu kuanzishwa kwa mtangamano
wa SADC.
“Hadi sasa hali ya amani na usalama
imeendelea kuimarika katika SADC kama inavyojidhihirisha kwa takribani
nchi zote za SADC ambapo nchi wanachama ziliazimia kusimamia maendeleo
ya kiuchumi ya Kanda kwa kuzingatia malengo ikiwemo kukuza uchumi,
kuondoa umasikini, kuboresha hali ya maisha ya wananchi.
Msingi wa SADC ni kusimamia malengo yake
ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii sambamba na yale ya ulinzi na
usalama unabainishwa katika Ibara ya 2 ya mkataba wa SADC ( Article 2 of
SADC Treaty).
0 comments:
Post a Comment