METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, December 21, 2017

Michuano ya Kusaka Vipaji Yazinduliwa Mwanza

Judith Ferdinand, Mwanza
Vilabu 20 vya soka mkoani Mwanza vimejitokeza kushiriki katika mashindano ya mpira wa miguu wa vijana chini ya umri wa miaka 12 na 15, ambayo yamezinduliwa juzi yenye lengo la kuibua vipaji.
Akizungumza na BMG, Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya wa Nyamagana (NDFA), Daddy Girbert wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, kwenye uwanja wa Nyamagana alisema, lengo la kuanzisha mashindano haya kipindi cha likizo ni  kuibua vipaji kwa watoto wa shule za msingi na sekondari
Dady alisema katika mashindano hayo  mwitikio ni mkubwa na ushindani ni mzuri kwani timu 20 zimejitokeza ambapo chini ya umri wa miaka 12 zipo tano na  umri wa miaka 15 zipo kumi na tano, hivyo  malengo ni kuhakikisha tasnia ya mpira wa miguu  mkoanj Mwanza inakua vizuri kuanzia kwa watoto.
“Tutafanya uchaguzi ili kupata vijana wenye vipaji ambao  watapata mafuzo maalumu ya sayansi ya mpira   na ufundi, kupitia klini ambayo itakuwa ikifanyika mara tatu kwa wiki kwa wale wenye  umri chini ya miaka  15 na wenye   miaka12  watafanya  mara mbili,”alisema Dady.
Pia alisema wale watakao kuwa tayari wamechaguliwa na kupewa nafasi ya kufanya mazoezi watajazwa katika database za vyama vya mpira wilaya na Mkoa,ili kijana atakapopata  fursa ya kwenda au  kuchaguliwa kushiriki katika ligi yoyote tutakuwa na taarifa zote muhimu zinazomhusu,  kwani kutasaidia kuondoa masuala ya ubabaishaji wa  kufoji umri.
Aliongeza kwa kufanya hivyo  wataweza kulinda vipaji vya watoto hao sambamba na  kuwapa  mafunzo  stahiki ya kujitambua kuwa anakipaji ili aweze kukitunza na  kukifanyia kazi.
Katika ufunguzi wa mashindano hayo timu ya Kona FC ya chini ya miaka 15 ilianza vizuri kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wapinzani wao Mwanza city,  huku timu ya Marsh Academy ikitoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya  Pamoja FC.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com